Home Kimataifa OKLAHOMA CITY THUNDER WAENDELEA KUPOROMOKA, CHICAGO BULLS YAWAKALISHA

OKLAHOMA CITY THUNDER WAENDELEA KUPOROMOKA, CHICAGO BULLS YAWAKALISHA

753
0
SHARE

ROSRose alikuwa katika kiwango kizuri na bora sana akifunga pointi 29, na Jimmy Butler aliongeza 26 na kuiongoza Chicago Bulls kuibuka na ushindi wa 104-98 dhidi ya  Kevin Durant na Oklahoma City Thunder Alhamisi usiku.

” Kwa upande wake kuwa  na mchezo mzuri kama huu, najua hii itakuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa kujiamini kwake, ” kocha Fred Hoiberg alisema. Bulls wamerudi mchezoni baada ya kutoka kupoteza kwa Charlotte Hornets kwa pointi 130-105.

Rose , bado amevaa kinyago usoni baada ya kukosa karibu preseason nzima kwa sababu ya kuvunjika upande wa kushoto wa uso. Hii ni baada ya kushindwa kucheza vyema katika michezo iliyopita huku akifunga pointi zisizozidi 10 katika michezo 3 mfululizo.

” Mchezo uliopita ilikuwa aibu kidogo ,” Rose alisema. “Ukiangalia marudio baada ya kilichotokea , tulihisi kuchanganyikiwa . Tuliona kama kila mmoja alimuangusha mwenzie. Baada ya mazoezi ya jana, tunaweza kusema tulirudisha ari na roho ya kipiganaji na kiushindani tena.

Russell Westbrook alikuwa na pointi 20 na pasi 10 kwa Oklahoma City, na Serge Ibaka alifunga 17.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here