Home Kimataifa TORONTO RAPTORS ILEEE, YAPATA USHINDI WA TANO MFULULIZO, YAIBABUA OKLAHOMA CITY THUNDER

TORONTO RAPTORS ILEEE, YAPATA USHINDI WA TANO MFULULIZO, YAIBABUA OKLAHOMA CITY THUNDER

461
0
SHARE

demarDemar DeRozan alifunga 10 ya pointi zake 28 katika robo ya nne , na Raptors wakatoka nyuma kwa pointi nane na kwenda kupata ushindi ndani ya dakika sita za mwisho. Toronto Raptors ikipata ushindi wake wa tano mfululizo kwa kuipiga Oklahoma City Thunder 103-98 Jumatano usiku.

” Mimi sijui na sina uhakika ni michezo mingapi tutashinda lakini najua kwamba tunakwenda na tutaendelea kufanya vyema,” kocha Dwane Casey alisema.  “Tutaendelea  kushindana, kucheza kwa bidii , kupata ubora wa  watu wetu.

Leo mitupo yetu haikuwa vyema na hatukupata vizuri lakini tuliamua kushambulia goli na kupata mitupo huru  na kufunga kutoka katika mstari. Ilibidi tuwalazimishe waamuzi wafanye maaamuzi kimchezo na safu ya ulinzi kufanya kazi yake.

Jonas Valanciunas alikuwa na pointi 17 na 12 rebounds na Kyle Lowry aliongeza pointi 17 kwa Raptors ( 5-0 ) , ambao wametoka kuwafunga Dallas Mavericks.

“Ni mambo yanayorekebishika,” nyota wa Oklahoma  Kevin Durant alisema. “Sina wasiwasi hata kidogo. Hii haimaanishi kuwa sisi hatuwezi kupata mtego au kuokoa juu haya yanayokwenda vibaya . Tunapoteza mipira sana, tunafanya madhambi sana, lakini yote ni sehemu ya mpira.

Russell Westbrook alifunga 20 ya pointi zake 22 katika kipindi cha pili na kumaliza na pasi 16 . Durant alikuwa na pointi 27 na Enes Kanter aliongeza 15 kwa Oklahoma City Thunder (3-2).

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here