Home Kimataifa SASA RASMI FILAMU YA RONALDO KUZINDULIWA NOVEMBA 9 MWAKA HUU.

SASA RASMI FILAMU YA RONALDO KUZINDULIWA NOVEMBA 9 MWAKA HUU.

526
0
SHARE

Ronaldo 1Baada ya sintofahamu ya muda mrefu juu ya lini filamu ‘movie’ ya Cristiano Ronaldo itatoka hatimaye filamu hiyo kuzinduliwa mwezi huu tarehe 9 na kuoneshwa na majumba mbalimbali ya sinema duniani.

Moja kati ya vipande vya filamu hiyo vinamuonesha mama wa Ronaldo Maria Dolores dos Santos Aveiro akiweka wazi kuwa alitaka kutoa ujauzito wa Ronaldo.

Akinukuliwa katika kipande hicho mama wa Ronaldo anasema “nilitaka kutoa ujauzito wa Ronaldo lakini Mungu hakutaka iwe hivyo.

Ronaldo hakuwa akihitajika kwangu kwa sababu nilitaka kuutoa ujauzito wake lakini mpaka sasa amenifanyia mambo makubwa” anamalizia mama wa Ronaldo Maria Dos Santos.

Filamu hiyo itakuwa na vipande tofauti tofauti vikielezea maisha ya Ronaldo pamoja na familia yake na imemchukua miezi 14 kutengeneza filamu hiyo.

Pia filamu ya Ronaldo itamzungumzia baba yake Ronaldo anayefahamika kama José Dinis Aveiro.Baba yake Ronaldo alikuwa akifanya kazi ya kutunza bustani katika manispaa ya Funchal katika mji wa Medeira lakini alikuwa ni mlevi sana.

Angalia kipande cha filamu yake mpya

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here