Home Kimataifa LEO KATIKA TBT:ALESSANDRO DEL PIERO APIGIWA MAKOFI BERNABEU

LEO KATIKA TBT:ALESSANDRO DEL PIERO APIGIWA MAKOFI BERNABEU

743
0
SHARE
Juventus' forward Alessandro Del Piero salutes after the final of the Cup of Italy Juventus vs Napoli at the Olympic Stadium in Rome on May 20, 2012. Napoli defeated Juventus by 2-0 to win the Cup. AFP PHOTO / GABRIEL BOUYS (Photo credit should read GABRIEL BOUYS/AFP/GettyImages)

Siku zote kumbukumbu ni sehemu ya maisha yetu sisi binadamu na uwepo wake hutufanya tuwe na furaha na amani katika maisha yetu ya kila siku.Tarehe kama ya leo ya 5/11/2008 kulikuwa na mchezo mkubwa sana katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mchezo huo ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya kibibi kizee cha Turin klabu ya Juventus.Kocha wa Real Madrid wakati huo alikuwa ni Bernd Schuster huku kocha wa Juventus akiwa ni kocha wa sasa wa klabu ya Leicester City ya nchini England Claudio Ranieri.

Mechi hiyo itaendelea kuwa  kumbukumbu kwa mshambuliaji na nahodha wa zamani wa klabu ya Juventus Alessandro Del Piero kwa kufunga magoli mawili katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Tukio kubwa katika mchezo huo ni kitendo cha mashabiki wa Real Madrid kumpa heshima ya kumpigia makofi Del Piero wakati anatoka nje kumpisha beki wa kushoto Paolo De Ceglie.

Ni wachezaji wachache sana waliowahi kupata heshima hiyo katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Wachezaji hao ni pamoja ni pamoja na Ronaldinho Gaucho alipofanyiwa hivyo mwaka 2009 katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Barcelona.

Katika mchezo huo,Ronaldinho alifunga magoli 2 katika ushindi wa Barcelona wa magoli 3-0 mbele ya Real Madrid.


Mchezaji mwingine alikuwa ni Diego Maradona wakati huo akiwa na klabu ya Barcelona katika mchezo dhidi ya Real Madrid 1983.

Kumbuku za kushangiliwa kwa wachezaji hawa zitaendelea kuwepo katika vichwa vyetu hasa Alessandro Del Piero kwa kuwa tunamkubuka kwa kufunga magoli mazuri tarehe kama ya leo ya 5/11/2008.

Vikosi vya timu za Real Madrid dhidi ya Juventus vilikuwa;

Madrid: Casillas; Ramos, Cannavaro, Heinze (Saviola), Marcelo; Diarra, Sneijder (Higuain), Guti, Drenthe; Raul, Van Nistelrooy (Van der Vaart)
Juve: Manninger; Mellberg, Legrottaglie, Chiellini, Molinaro; Marchionni, Tiago, Sissoko, Nedved; Amauri (Iaquinta), Del Piero (De Ceglie)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here