Home Ligi EPL Cristiano Ronaldo ana ndoto za kurejea Old Trafford 2016

Cristiano Ronaldo ana ndoto za kurejea Old Trafford 2016

662
0
SHARE

Tangu alipoondoka Old Trafford mnamo mwaka 2009, kujiunga na Real Madrid, tetesi za kurejea katika klabu iliyompa umaarufu zaidi duniani – Manchester United hazijawahi kukoma.

  Mwanasoka anayeshikilia tuzo ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo amezidi kuzikoleza tetesi hizo baada ya kuripotiwa kwamba ana ndoto za kurejea Old Trafford na aliwaambia wachezaji wenzie wa Los Blancos mwaka 2014 kwamba anaimani atarejea Old Trafford ndani ya miaka miwili ijayo, hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Hispania Guillem Balague.

Katika kitabu kipya kinachohusu maisha ya Cristiano Ronaldo, mwandishi Balague anatoa ishara kwamba United bado wamebaki kwenye moyo mwanasoka huyo na anafikiria sasa kurejea kuitumikia klabu aliyoihama mwaka 2009. 

  Cristiano Ronaldo bado ana ndoto za kurejea kuvaa jezi za Manchester United. Klabu hii ya Uingereza ilimtaarifu wakala wa mchezaji kwamba wana misuli ya kuiwezesha kurudi kwa Ronaldo Trafford. 

Kila kitu kinaelezwa kimeshawekwa tayari siku nyingi kwa usajili wa Ronaldo ikiwa Madrid na Man United wataamua kufanya biashara hiyo. 

Pamoja na kwamba Ronaldo atakuwa anatimiza miaka 31 mwezi February, bado atakuwa anauzwa kwa bei kubwa. 

Ronaldo ana mkataba na Madrid ambao unamalizika mwaka 2018. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here