Home Kitaifa AZAM FC WATAFANYA TENA WALICHOWAHI KUFANYA?

AZAM FC WATAFANYA TENA WALICHOWAHI KUFANYA?

440
0
SHARE

aas

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Kufanikiwa kwenye msimu maalum mara zote ni kitu cha kustaajabisha na kufurahisha, kufanikiwa kwenye misimu misimu miwili ni kitu cha kipekee zaidi. Ligi kuu Bara ina mifano baadhi, timu kung’aa msimu mmoja na kupotea.

Mabingwa ligi miaka ya 1999 na 2000 Mtibwa Sugar, makamu bingwa wa ligi kuu 2002 na 2008 Tanzania Prisons, makamu bingwa wa ligi 2006 Moro United hadi kwa Mbeya City FC, timu hizi zilikuwa imara sana katika miaka Fulani ndani ya miaka hii 15 lakini zimeporomo uwezo.

Baadhi zinakuwa hadi chini ya nusu ya timu katika ligi. Wapi Azam FC watakapokuwa kwa muda wa miezi Mitano ijayo?. Hakuna aliyetaraji timu hiyo iliposhinda ubingwa msimu wa 2013/14 na kwa misimu mitatu kati ya minne iliyopita wamefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili. Swali la kujiuliza, je, wataweza kuendelea kuifuata njia yao?

Tayari wameshinda ubingwa wa klabu Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, 2015 na hadi sasa wanashikilia usukani wa ligi wakiwa na alama 25 baada ya kucheza game 9. Wameshinda mara Nane na kulazimishwa sare mara moja. Wapo katika utaratibu waliouanzisha tangu msimu wa 2011/12 walipofanikiwa kuingia nafasi mbili za juu ( wakati ule wakiipiga kumbo Yanga SC).

Sasa kila timu itataka kuishinda Azam FC kwa mara ya kwanza baada ya kucheza game 15 mfululizo pasipo kupoteza. Walishinda Kagame Cup baada ya kucheza mechi 6 mfululizo pasipo kupoteza, huku wakifanya hivyo mara 9 katika VPL. Hakutakuwa na cha kushtusha. Lakini timu ya kwanza kuishinda Azam FC itapaswa kuwa na ‘ kiwango’ cha juu na si kubahatisha.

Watacheza na Simba SC mwezi Disemba kisha gemu ambayo watakuwa wenyeji, kisha Majimaji FC ugenini, Kagera Sugar na Africans Sports-nyumbani. Kila timu inatamani kuwafunga wao lakini ni lazima wafuatilie vile Kipre Tchetche anavyotembea na mipira, Shomari Kapombe anavyofunga na kutengeneza nafasi za magoli, jinsi gani Paschal Wawa hulinda. Watacheza FA Cup, kombe la Shirikisho lakini kampeni yao ni kushinda ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya pili msimu huu.

Stewart Hall amerudi kwa mara ya tatu kama mkufunzi wa timu hiyo na kwa kikosi alichokijenga mwenyewe. Aishi Manula, Kapombe, Said Mourad, Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao, Salum Abubakary, Kipre Bolou, Pierre Mugiraneza ‘ Migi’, Kipre, John Bocco, Didier Kavumbagu, Allan Wanga, Ramadhani Singano, Farid Musa, Mudathir Yahya, David Mwantika, Gadiel Michael wote ni wachezaji wa kutegemewa katika timu.

Hall amepata baadhi ya vijana kama Farid, Mudathir, Singano ambao wana ‘ njaa’ na ‘ wanyumbulifu’. Usajili wa Wanga bado haujalipa lakini mchezaji huyo amekuwa akiongeza uzoefu katika safu ya mashambulizi. Ushawishi wa Wawa katika safu ya ulinzi, ujio wa Migi katika kiungo, Singano, Wanga katika mashambulizi unaongeza hamasa ya kuungana na wachezaji wengine kufanikisha mapinduzi mengine ya Hall baada ya kushinda Kagame Cup.

Licha ya kushindwa mara mbili kushinda ubingwa wa VPL akiwa mkufunzi wa Azam FC misimu ya 2011/12, 2012/13 mara hii Hall hawezi kushindwa na atamaliza tena nafasi zile zile ambazo Azam FC wamekuwa wakimaliza katika misimu minne iliyopita. Azam FC watafanya tena walichofanya 2013/14?. Wakithubutu, watafanya kwani hadi sasa ndiyo vinara wa ligi kuu msimu wa 2015/16.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here