Home Kimataifa AFRICA INAWEZA KUWEKA HISTORIA KWENYE KOMBE LA DUNIA

AFRICA INAWEZA KUWEKA HISTORIA KWENYE KOMBE LA DUNIA

533
0
SHARE

fifa

Baada ya mechi za leo kwenye kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17, Africa inaweza kuweka historia kwa nchi mbili za Africa kucheza fainali za kombe la dunia.

Mechi za leo ni nusu fainali kati ya Nigeria Vs Mexico na Mali Vs Belgium, baada ya mechi kuisha kama Nigeria ikimfunga Mexico na Mali ikamfunga Belgium basi fainali itakua kati ya Nigeria Vs Mali.

Nigeria inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kwasababu wana mfungaji bora wa michuano na pia wameitoa timu kama Brazil. Michuano hii inafanyika huko Chile na kwa hapa nyumbani inaonekana live kupitia king’amuzi cha Startimes. Usipiwe na uhondo huu uone jinsi vijana wanavyoonyesha njaa ya kutaka kupata mafanikio kwenye soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here