Home Dauda TV VIDEO: MASKINI ARSENAL!! YACHINJIWA BAHARINI

VIDEO: MASKINI ARSENAL!! YACHINJIWA BAHARINI

473
0
SHARE

Bayern Munich

Timu ya Arsenal imejikuta ikipokea kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa mabingwa wa Ujerumani timu ya Bayern Munich ‘The Bavarians’ kwa kusukumiwa goli 5-1 ikiwa ni mwendelezo wa mechi za vilabu bingwa Ulaya hatua ya makundi mchezo uliopigwa kwenye dimba la Allianz Arena, Ujerumani.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Bayern ikiwa inaongoza kwa magoli 3-0, magoli yaliyofungwa na Robert Lewandowsk, Thomas Muller na David Alaba .

Kipindi cha pili bado Bayern Munich waliendeleza mvua ya magoli, Arjen Robben aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Coman alipachika bao la pili kabla ya Thomas Muller hajakamilisha ushindi wa goli 5 kwa upande wa Bayern.

Goli pekee la Arsenal limefungwa na Olivier Giroud

Arsenal imebaki na pointi tatu baada ya kucheza mechi nne ikiwa nyuma ya Bayern Munich na Olympiakos kwa ponti sita wakati imebaki michezo miwili ya hatua ya makundi.

Olympiakos wameibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Dinamo Zagreb na kufifisha matumaini ya Arsena kufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here