Home Kitaifa UWANJA WA AMAAN WAPIGWA KUFULI, HAKUNA CHA LIGI KUU WALA LIGI ZA...

UWANJA WA AMAAN WAPIGWA KUFULI, HAKUNA CHA LIGI KUU WALA LIGI ZA WILAYA, HATA NDONDO

641
0
SHARE
Muonekano wa uwanja wa Amaan kwa juu
Muonekano wa uwanja wa Amaan kwa juu
Muonekano wa uwanja wa Amaan kwa juu

Na Abubakar Kisandu

Chama cha soka cha wilaya ya mjini leo kimethibitisha kupokea barua kutoka kwa kaimu meneja wa uwanja wa Amaan kwa kutakiwa kutoutumia uwanja huo mpaka watakapoambiwa.

Akizungumza kwa masikitiko mwenyekiti wa ZFA wilaya ya mjini Hassan Haji Hamza ‘Chura’ amethibitisha kwa kupokea barua hiyo lakini wao kama ZFA wilaya ya mjini wamesema watafatilia zaidi kwanini wasicheze wao na uzuiliwe wakati shughuli za uchaguzi wa nchi zimeshatulia.

Amesema ikiwa kweli hata serikali wataunga mkono hilo la kutotumiwa uwanja huo watakaa na vilabu vyao ili wajue nini watafanya na ligi yao ichezwe.

Hatukuishia hapo tukamtafuta kaimu meneja wa uwanja wa Amaan Simai Mohamed Mavuni kwa kutaka kujua kwanini amesitisha kutumiwa uwanja wa Amaan.

Sehemu ya mbele ya uwanja wa Amaan
Sehemu ya mbele ya uwanja wa Amaan

Simai amesema amesitisha kutumika uwanja huo kwasababu bado hali ya usalama haijakaa sawa visiwani Zanzibar na vikundi havitakiwi kwa kuja uwanjani hapo kaungalia mpira.

Aidha Simai amesema yeye anapenda michezo kuliko viongozi waliopo sasaivi lakini kasitisha kutokana na hali ya nchi tu.

“Kutokana na umri wangu mimi napenda michezo kuliko hata viongozi wanaoongoza sasaivi mana kila siku wanapelekekana mahakamani”.

Aidha meneja huyo amesema hakusitisha mpira wa miguu tu pekee bali hata michezo mingine ikiwemo riadha na nk.

Sehemu wa VIP ya uwanja wa Amaan
Sehemu wa VIP ya uwanja wa Amaan

Kuhusu mpaka lini uwanja huo utatumika Simai amesema inaweza kufika wiki tatu au mwezi au zaidi ya hapo.

Amewaomba wadau wa michezo wanaotumia uwanja huo wastahamili kwa kipindi hiki kigumu kwani kufanya hivyo ndio kuulinda uwanja huo.

Ligi kuu soka Zanzibar inatarajiwa kutimua vumbi lake November 10 mwaka huu ambapo kutokana na taarifa ya kaimu meneja wa uwanja wa Amaan huenda ikachezwa mwituni (Viwanja vidogovidogo) kwani hata uwanja wa Mao Tsi Tung upo kwenye matengenezo.

Uwanja wa Amaan unachukua jumla ya Watazamaji  15,000 ambapo pia ndiyo uwanja mkuu wa michezo Zanzibar , ukiwemo mpira wa miguu kama lakini hata riadha  na mambo mengine zikiwemo sherehe hasa za Mapinduzi Januari 12 kila mwaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here