Home Dauda TV VIDEO: ROONEY AFUFUKA MAN UNITED IKIPATA USHINDI WA NYUMBANI

VIDEO: ROONEY AFUFUKA MAN UNITED IKIPATA USHINDI WA NYUMBANI

411
0
SHARE

Wayne Rooney UEFA

Mshabuliaji wa Manchester United Wayne Rooney aliifungia timu yake bao pekee wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye uwanja wa nyumbani (Old Trafford) wakati ilipoikaribisha timu ya CSKA Moscow kwenye mchezo wa UEFA Champions League uliochezwa usiku wa Jumanne November 3.

Rooney alifunga goli hilo dakika ya 79 kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na kijana chipukizi Jesse Lingard ambaye ndiye alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Rooney UEFA 1

Ushindi huo umeifanya United kufikisha jumla ya pointi saba na kukaa kileleni mwa kundi B huku ikiwa bado inamichezo miwili mkononi baada ya Wolfsburg ambao walikuwa wakiongoza kundi hilo wakiwa na pointi sita kupokea kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa PSV Eindhoven.

Rooney UEFA 2

Angalia video ya goli ambalo limefungwa kwa kichwa na Wayne Rooney dakika za lala salama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here