Home Kimataifa Usiku wa Ulaya: Nani kuingia 16 bora, nani kuaga Mashindano leo?

Usiku wa Ulaya: Nani kuingia 16 bora, nani kuaga Mashindano leo?

669
0
SHARE

Usiku wa ulaya unaokutanisha vilabu mabingwa wa ulaya unaendelea leo kwa michezo 8 kupigwa katika viwanja tofauti barani humo.

  
Usiku wa leo ndio hatua ya makundi inaingia mzunguko wa pili lakini baada ya mechi za leo na kesho timu kadhaa kwenyw kundi la timu 32 zitakuwa zimeshafahamu hatma yao.

Wakati mabingwa watetezi FC Barcelona na timu nyingine pekee ambayo imeshinda mechi zote Zenit ni miongoni mwa timu ambazo zinaweza kufuzu kwenda raundi ya 16 bora baada ya mechi za wiki hii, Shakhtar Donestski na Sevilla wao wapo miongoni mwa timu zinazoweza kuaga mashindano. 

Group A: Real Madrid (7pts) v Paris Saint-Germain (7), Shakhtar Donetsk (0) v Malmö (3) 

 •Ikiwa aidha Paria au Madrid mmoja akishinda, basi atafuzu endapo tu Malmo watapoteza mchezo wa leo.
•Kama Shakhtar watapoteza mchezo wa leo au endapo mechi za leo za Kundi A zote zikiwa sare basi moja kwa moja timu ya Ukraine itashindwa kumaliza ndani ya Top 2 na hivyo kushindwa kufuzu. 

Group B: Manchester United (4) v CSKA Moskva (4), PSV Eindhoven (3) v Wolfsburg (6) 

 •Kwa bahati nzuri kwenye kundi hili hakuna timu inayoweza kufuzu au kuondolewa kwenye mashindano baada ya mechi za leo na kesho. 
•Group C: Astana (1) v Atlético Madrid (6), Benfica (6) v Galatasaray (4) 

 Ikiwa Astana watapoteza mchezo wa leo na Benfica wakashinda, basi Astana hawawezi kumaliza ndani ya nafasi mbili za juu. 

Group D: Borussia Mönchengladbach (1) v Juventus (7), Sevilla (3) v Manchester City (6) 

 •Kama  Juventus na City watashinda, wote watakuwa wamefuzu moja kwa moja na Sevilla watapambana na Mönchengladbach kugombea nafasi ya 3. 

•Ikiwa City watashinda na michezo mingine kwenye kundi – City watakuwa wamepita. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here