Home Ligi EPL REFEREE AJIKUTA AKISHANGILIA GOLI LA TOTTENHAM

REFEREE AJIKUTA AKISHANGILIA GOLI LA TOTTENHAM

604
0
SHARE

Mike Dean 1

Baada ya mchezo wa jana kati ya Tottenham dhidi ya Aston Villa uliochezwa kwenye uwanja wa White Hart Lane, kumeibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamemtuhumu mwamuzi Mike Dean aliyechezesha mchezo huo kuwa alishangilia goli la kwanza lililofungwa na Mousa Dembele.

Dean alimpa ‘advantage’ Dembele kabla ya kufunga goli hilo ambalo lilikuwa la kwanza kwa Tottenham, Dean alionekana kwenye picha za video kama anashangilia goli hilo.

Madai hayo yameunganishwa na matukio ya nyuma ya mwamuzi huyo yanayoihusu Tottenham ambapo mara kadhaa ameonekana akichukizwa endapo amempa advantage mchezaji wa timu hiyo halafu akapoteza mpira lakini mara kadhaa amekuwa akihusishwa kuipendelea timu hiyo na mara nyingine kushangilia magoli yanayofungwa na Tottenham.

Lakini baadhi ya wadau wa soka wanadai kuwa mwamuzi huyo amekuwa akifurahishwa na matukio mazuri uwanjani bila kujali timu gani imefanya tukio ambalo limemvutia Dean.

January 2014 wakati Manchester United inacheza mchezo wa FA Cup dhidi ya Swansea City kwenye uwanja wa Old Trafford, Dean alionekana kutoridhishwa na Swansea kushindwa kutumia vyema advantage aliyowapa.

Lakini mwaka 2012 inadaiwa Dean alishindwa kujizuia na akajikuta akishangilia goli la Luis Saha lilofungwa kwenye mchezo wa London Derby kati ya Arsenal dhidi ya Tottenham.

Hii hapa video inayoonesha madai kuwa Mike Dean anashangilia goli lililofungwa na Mousa Dembele wakati Tottenham ikiibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Aston Villa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here