Home Kimataifa NANI ATAMFUNGA STEPHEN CURRY KENGELE, GRIZZLIES WAFA KIFO KIBAYA.

NANI ATAMFUNGA STEPHEN CURRY KENGELE, GRIZZLIES WAFA KIFO KIBAYA.

478
0
SHARE

CURRStephen Curry alifunga 21 ya pointi zake 30 katika robo yan tatu ya mcjhezo akiendeleza ubora wake na kudhihirisha kwanini alikuwa  NBA MVP. Hii ikiwa ni baada ya kufunga point  53 katika mchezo uliopita dhidi ya New Orleans Pelicans, na  Warriors wameivurumisha  Memphis Grizzlies 119-69.

Mepmphis Grizzlies imeshuhudia rekodi yao mbovu zaidi katika Historia ya NBA baada ya kufungwa kwa tofauti ya point 50 na Warriors, huku rekodi iliyokuwepo ikiwa ni kufungwa kwa tofauti ya point 49 hiyo ikiwa waka 1995, kipindi hicho inaitwa Vancouver Grizzlies.

Stephen Curry hakucheza katika robo ya nne kabisa  huku timu yake ikiongoza kwa kaisi kikubwa,na alipata mitupo 10 kati ya 16 aliyojaribu ikiwemo point 3 nne. Mpaka sasa amefunga point 3 mara 21 katika michezo 4 msimu huu. Mapema kabla ya mchezo kocha wa  Grizzlies David Joerger aliongea kwa mzaha, “tunskwenda kumuwekea watu 3 wa kumkaba leo”

Timu zote ambazo Warriors imezifunga mpaka sasa katika michezo 4 ambazo ni Pelicans, Houston na Memphis ndizo ambazo ilizitoa katika hatua ya mtoano katika kanda ya Magharibi na hatimaye kushinda uchampion wa NBA.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here