Home Kitaifa KUNA YE YOTE ANAYEWEZA KUIZUA YANGA SC?

KUNA YE YOTE ANAYEWEZA KUIZUA YANGA SC?

499
0
SHARE

yanga

NA Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Ligi kuu ya Tanzania Bara itasimama kwa muda hadi mwezi Disemba kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo Novemba 14 itacheza mchezo wa kwanza hatua ya mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2018-Urussi. Stars itacheza na timu ya Taifa ya Algeria baada ya kufanikiwa kuwaondoa timu ya Taifa ya Malawi.

Kuna ye yote anaweza kuizuia Yanga SC? Vizuri, yeyote anaweza kujaribu na akaweza. Lakini baada ya kuiangalia Yanga katika gemu 9 msimu huu, wakiitawala Simba na kuichapa 2-0, Mtibwa Sugar 2-0, kisha wakalazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC . inaonesha kama mabingwa hawa watetezi wamedhamilia ‘ kumaliza biashara mapema’. Yanga haijawahi kuwa na mwanzo hivi.

Ushindi mara 7, sare mara mbili katika michezo tisa ya msimu huu. Msimu uliopita, Yanga ilifaidika na ‘ mseleleko wa klabu za Simba, Mbeya City, Azam na Mtibwa Sugar. Licha ya kupoteza michezo mitano kati ya 26 kikosi cha Hans Van der Pluijm kiliweza kushinda gemu zote ngumu ambazo wapinzani wao walishindwa kushinda.

Licha ya kufungwa na Simba na Azam katika gemu za merejeano, Yanga ilifanikiwa kushinda ubingwa wa 24 licha ya kuambulia alama mbili tu katika mipambano minne dhidi ya klabu hizo mbili. Mtibwa Sugar, Kagara Sugar na Ndanda FC ni timu nyingine tatu ambazo ziliifunga Yanga msimu uliopita, lakini msimu huu tayari Yanga imefanikiwa kuzishinda timu tatu kati ya tano zilizowafunga msimu uliopita.

Jumamosi iliyopita waliweza kuifunga Kagera Sugar kwa magoli 2-0 ugenini katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora na hivyo kufikisha alama 23, pointi mbili nyuma ya Azam FC wanaoshikilia usukani wa ligi.

Dhahiri Yanga wamependa ‘ mwanzo wao huu’ wakiwa imara. Kikosi kina mabadiliko kiasi. Hasa safu ya mashambulizi lakini dhahiri timu ni ile ile. Donald Ngoma amefanya vizuri hadi sasa. Akiwa tayari amecheza mechi tisa za ligi kuu bara raia huyo wa Zimbabwe ameweza kutengeneza ushirikiano mkubwa na Mrundi, Amis Tambwe.

Ngoma amekwishafunga mara Tisa msimu huu, Tambwe amefunga mara Tano wakati mfungaji bora wa msimu uliopita Saimon Msuva akiwa amekwishafunga mara tatu. Mshambuliaji mwingine mpya katika timu hiyo Malimi Busungu ‘ si haba’ licha ya kufunga mabao mawili amekuwa na mchango mkubwa sana katika timu yake kwa upatikanaji wa magoli. Yanga imefunga magoli 18 ( idadi ya juu zaidi kwa timu msimu huu).

Ngoma ni kama amechukua nafasi ya Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free Staste Stars ya Afrika Kusini na kuitendea haki. Busungu amekuwa na msaada mkubwa zaidi ya uwepo wa awali wa Said Bahanunzi, Hussein Javu na Jerry Tegete. Yanga imefanikiwa kufunga goli/magoli katika kila mchezo. Wastani wao wa ufungaji kwa mechi ni magoli mawili.

Lakini kwa Thaban Kamusok o, Yanga walitaka kumuongeza mchezaji mwingine mwenye kiwango cha kimataifa. Uwepo wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na viungo hodari ‘ wazawa’ Salum Telela, Said Juma ‘ Makapu’, wakati mwingine Mnyarwanda, Mbuyu Twite umemfanya Hans kuwa na machaguo manne hadi matano ya uhakika katika sehemu ya kiungo wa kati.

Deus Kaseke alianza vizuri kabla ya kufifia kiasi lakini kiwango chake alichokionesha katika game dhidi ya Kagera ni kielelezo tosha kuwa Yanga ina timu kubwa yenye wachezaji wasiotofautiana uwezo. Kaseke alifunga kwa mara ya kwanza katika ligi kuu akiwa na Yanga dhidi ya Kagera Sugar ni wing mwenye uwezo wa kubeba majukumu ya kiungo wa mashambulizi pia. Yanga pia ina mawing wawili vijana, Mbrazil, Andrey Coutinho na Geofrey Mwashuiya.

Ikiwa imeruhusu magoli manne hadi sasa, safu ya ulinzi ya Yanga imemuongeza raia wa Togo, Vicent Bossou ambaye alicheza gemu yake ya pili ya VPL dhidi ya Kagera Sugar. Hans aliwalalamikia walinzi wake wa kati, nahodha wa timu, Nadir Haroub na Kelvin Yondan baada ya kuruhusu Mwadui FC kusawazisha mara mbili alifanya mabadiliko katika game ya Jumamosi iliyopita na Vicent aliweza kucheza vizuri.

Juma Abdul amecheza namba mbili kwa umakini mkubwa, tayari ametengeneza mabao mawili na kufunga moja, upande wa kushoto kijana mpya, Hajji Mwinyi ameendelea kucheza kwa kujiamini licha ya kuwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya Bara. Nani wa kuisimamisha Yanga SC msimu huu isitetee ubingwa wake?. Kila timu inaweza, ikithubutu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here