Home Kitaifa KAMARI ZA USAJILI ZIMELIPA VPL?

KAMARI ZA USAJILI ZIMELIPA VPL?

663
0
SHARE

Benchi

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Bila shaka uhamisho mkubwa wa majira ya kiangazi, Tanzania bara ni uhamisho wa Vicent Bossou mlinzi wa kati raia wa Togo ambaye amesajiliwa na Yanga SC. Mchezaji huyo amecheza dakika 180 tu katika gemu tisa za Yanga katika ligi kuu. Lakini kulikuwa na maingizo mengine yenye kuleta mvuto kwenye  ligi kuu bara.

Usajili wake ni ghali kwa kuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu yake, pia anavuta mshahara mkubwa zaidi VPL. Vicent ni pendekezo la mkufunzi mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans Van der Pluijm usajili wake ulikuwa ‘ukibezwa sana’ lakini baada ya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Toto Africans wengi walianza kumuamini mchezaji huyo.

Usajili wake bado unaweza kuuweka katika kipengele cha ‘Kamali Kubwa’. Lakini hadi sasa Yanga inafurahia usajili wa wachezaji wake, Mwinyi Hajji, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Malimi Busungu, Deus Kaseke, Ge ofrey Mwaishuiya ambao wanafanya vizuri sana.

Azam FC ilimsajili Mkenya, Allan Wanga na mshambuliaji huyo licha ya kuwa tayari amefunga katika ligi kuu bara, alishindwa kuonesha uwezo mkubwa katika mechi dhidi ya Yanga. Azam FC Ikiwa na washambuaji, Mu-ivory Coast, Kipre Tchetche, Mrundi, Didier Kavumbagu ambaye aliwafungia magoli 11 msimu uliopita, nahodha John Bocco, Ame Ally, Kelvin Friday nafikiri Azam FC ilichemsha kumsaini Wanga.

Kama kuna mchezaji aliye-fifia zaidi hadi sasa na alisajiliwa kwa matarajio makubwa basi ni Mkenya huyu. Pierre Mugiraneza ‘Migi’ pia ni usajili wa gharama ambao Azam iiiufanya wakati wa usajili uliopita.

Migi ameweza kuisaidia Azam kushinda ubingwa wa Kagame Cup na hadi sasa ameendelea kuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza. Ramadhani Singano amesajiliwa kwa dau kubwa baada ya kumaliza mkataba wake Simba. Je, kamari hizi za Azam FC zimewalipa?

Hadi sasa wanashikilia usukani wa ligi kuu, katika game tisa hawajapoteza mechi, zaidi ya kupata sare mara moja. Upande wa Simba. Peter Mwalyanzi, Mwinyi Kazimoto, Sam Hajji Nuhu, Mohamed Fakhi, Joseph Kimwaga ni baadhi ya wachezaji wazawa waliosajiliwa katika usajili uliopita. Mganda, Hamis Kiiza, Mzimbabwe, Justice Majabvi, Mrundi, Nimubona na kipa raia wa Ivory Coast, Vicent Aghban walisajiliwa kutoka nje ya nchi.

Kiiza amefanikiwa kufunga magoli nane (8) katika game tano alizoichezea timu yake, Majabvi pia amekuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza katika kila mechi. Usajili wa Kiiza na kiungo huyu mlinzi wa timu ya Taifa ya Zimbabwe umelipa vizuri hadi sasa. Mwalyanzi, Mwinyi wamefanya vizuri kwa wachezaji wa ndani katika timu hiyo ambayo inashikilia rekodi ya ushindi mkubwa zaidi katika ligi. Simba ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 21.

Baada ya kutemwa katika timu ya Simba, straika kijana Eluis Maguli haraka alisajiliwa na Stand United ya Shinyanga. Kilinachoendelea upande wake ni ‘furaha’ tu kwani tayari amefunga magoli tisa msimu huu na kuwa mchezaji mzawa aliyefunga magoli mengi hadi sasa. Kamari hii imelipa vizuri kwa Stand kwa kuwa walimsajili Maguli akiwa ametoka kufunga magoli manne tu katika msimu wa 2014/15.

Atupele Green kijana mwingine ambaye aliamua kuachana na Kagera Sugar na kujiunga na Ndanda FC. Green mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Ruvu Shooting ndiye mfungaji wa goli la kwanza msimu huu wakati Ndanda ilipolazimishwa sare ya kufungana 1-1 na JKT Mgambo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Septemba 12. Green amefunga magoli manne na kuwa kinara wa ufungaji katika timu yake.

Jerry Tegete amefanikiwa kufunga magoli matatu hadi sasa akiwa na Mwadui FC. Jerry alidumu Yanga tangu mwaka 2008 ameichezea Mwadui FC game tano msimu huu. Si yeye tu, timu hiyo ya Shinyanga imewasaini wachezaji mastaa kama Nizar Khalfan, Paul Nonga, Rashid Mandawa, Anthony Matogolo, Malika Ndeule, David Luhende, Jamal Mnyate, Jabir Stima, Razaq Khalfan.

Usajili huu bado unabaki katika ‘Kamari Kubwa’ kwa kuwa Mwadui tayari imepoteza game tatu huku kipigo cha 4-1 kutoka kwa Mtibwa Sugar kikiacha maswali mengi kwa wadau kuhusu uwezo halisi wa timu hiyo.

Coasta Union imefanikiwa kufunga magoli mawili tu licha ya kuwasajili washambuliaji Ally Shiboli, Mnigeria Chidibere  ambao hakuna yeyote aliyeweza kufunga hadi ligi inafikia mchezo wa kumi upande wao. ‘Kamari’ yao haina mategemeo bila shaka wanahitaji kufanya usajili zaidi katika safu yao ya mashambulizi.

Zahoro Pazzi, Nsa Job walisajiliwa na Africans Sports ili kuifanya timu hiyo kuwa na uwezo wa kufunga lakini kinachoendelea kwao ni ukame wa magoli katika timu. Sports imefunga goli moja tu katika game tisa ilizokwisha cheza. Nsa alikimbilia katika mambo ya siasa, Zahoro haonekani pia haonekani uwanjani.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here