Home Kitaifa Juma Ndanda Liuzio; Niliishi bila kuwa na Tsh.100 Mtibwa Sugar, sijui kwa...

Juma Ndanda Liuzio; Niliishi bila kuwa na Tsh.100 Mtibwa Sugar, sijui kwa nini nipo nje ya Taifa Stars.

590
0
SHARE

ZEEE

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Juma Ndanda Liuzio Jumamosi iliyopita aliisaidia klabu yake ya Zesco United kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Zambia ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii. Liuzio mwenye miaka 20 hivi sasa alisajiliwa na Zesco Julai mwaka 2014 akitokea klabu bingwa mara mbili ya zamani ya Tanzania Bara, Mtibwa Sugar.

Hilo ni taji lake la Tatu kushinda akiwa na mabingwa hao wa Zambia ambao walishinda mataji mawili msimu uliopita. Amecheza jumla ya mechi 19 na kufanikiwa kufunga magoli 6 huku aki-asisst mara 4 msimu huu. Ameshindwa kucheza game 11 kutokana na kupata majeraha wakati Fulani, pia majukumu ya timu ya Taifa yalichangia pia mchezaji huyo kushindwa kucheza mechi zote 30 za Zesco.

“Ushindani ulikuwa mkubwa kwa msimu wote, nashuku Mungu tumefanikiwa kushinda ubingwa wiki moja kabla ya kumalizika kwa msimu” anaanza kusema Liuzio wakati nilipofanya naye mahojiano Jumanne hii akiwa nchini Zambia.

Akiwa amecheza Zambia kwa mwaka mmoja sasa Liuzio amejitahidi kubaki katika mstali ambao anaamini anaweza kufanikiwa zaidi kimpira. Zambia kwa kawaida ni nchi ambayo matumizi ya Pombe ni ya kiwango cha juu hali hiyo imefanya baadhi ya vijana kutumia zaidi pombe na kujikuta wakisahau majukumu yao ya kikazi.

“Nimejifunza vitu vingi sana tangu nilipofika hapa kwa mara ya kwanza, huku wachezaji wengi ni walevi hivyo  huwa najiepusha nao sana. Wachezaji wengi wanaokuja kucheza hapa ( Zambia) wamejikuta wakishindwa kudumu kwa sababu hupenda kuiga maisha. Muda wangu mwingi nimekuwa nikiutumia kupumzika nyumbani” anasema mshambuaji huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ambaye amepangiwa nyumba kubwa nchini humo na klabu yake.

“Nina furaha kubwa  kupiga hatua kutoka nyumbani  Tanzania kuja hapa ila sina furaha ya kuwa hapa , kwa maana bado sijafikia malengo yangu. Furaha yangu ni kutoka hapa na kwenda mbele zaidi ya hapa kwenda kucheza katika timu kubwa zaidi ya Zesco.

Liuzio amekuwa na ‘ tamaa’ ya kucheza ligi kuu ya Afrika Kusini kwa kuwa anaamini kucheza katika ligi hiyo kutamuongezea nafasi ya kuonesha uwezo wake kwa klabu za barani ulaya ambazo huifuatilia sana ligi hiyo inayotajwa kuwa bora zaidi barani Afrika. Akiwa na wakala raia wa Qatar, Liuzio  amewataka Watanzania kuendelea kuwasapoti Vijana wao wanaocheza nje ya nchi na kuwatia moyo.

“Ningependa kuchukua nafasi hii kuwao Watanzania waendelee kutusapoti vijana wao ambao tupo nje ya mipaka yetu tukicheza mpira. Ni vyema wakasaidia kuwashawishi wachezaji wengine kwenda kucheza nje ya nchi ili idadi yetu iongezeke.”

Kwa sasa Tanzania ina baadhi ya vijana wanaofanya vizuri nje ya nchi. Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta tayari wameweka rekodi ya kuwa wacheza soka wa kwanza wa Tanzania kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Afrika. Wachezaji hao wa timu ya Taifa Stars walianza katika kikosi cha kwanza cha mabingwa mara nne wa kihistoria wa michuano TP Mazembe ya DR Conga siku ya Jumapili iliyoma wakati TP iliposhinda 2-1 ugenini dhidi ya USM Algers ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa fainali.

“Ni changamoto kubwa  kwa wachezaji wengine wa Tanzania. Kucheza fainali ya klabu bingwa Afrika si jambo rahisi. Hakika wanatupa ‘ challenge’ na sisi wengine kupambana kuhakikisha tunafikia mafanikio hayo. Ni ngumu kucheza fainali kubwa Afrika ukiwa na klabu za Tanzania, si rahisi kufika hata nusu fainali kwa kuwa mfumo wetu wa mpira hautengenezi mazingira ubora. Siku zote nitacheza kwa kujituma, nidhamu ili nitoke nje ya Bara hili la Afrika na kwenda timu kubwa za ulaya”

Liuzio hajaitwa katika timu ya Taifa Stars ambayo itacheza na Algeria katikati ya mwezi huu katika mechi za mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia nchini Urussi mwaka 2018. Tangu Charles Mkwassa alipochukua nafasi ya Mholanzi, Martin Nooij baada ya timu hiyo kuvurunda katika michezo ya Cosafa, kufuzu kucheza CAN 2017 na ile ya CHAN 2018 katikati ya mwaka huu.

“Kila ana mfumo wake na ana aina ya wachezaji ambaoatapenda kuwatumia hivyo inawezekana kwenye mfumo wa mwalimu wa sasa sihitajiki sana. Sina furaha kuwa nje ya timu kwa sababu siku zote napenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa” anasema Liuzio ambaye anakiri hajawahi kuzungumza na mwalimu Mkwassa wala msaidizi wake Hemed Morocco tangu walipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo.

Kwa nini Nooooij hakupata matokeo Gemu 18 kashinda 3 Tu…?

“Ilikuwa kila siku ni afadhali ya jana, mambo hayakuwa yakienda sawa katika timu. Wachezaji walikuwa wakicheza kwa kujitolea tu. Nakumbuka baada kucheza na Malawi wachezaji hawakuwa wamepewa posho hadi tunacheza na Misri. Tulipokuwa Afrika Kusini tulipewa posho na wadhamini wa timu-Kilimanjaro” anasema Liuzio

Wachezaji wa Stars wamekuwa wakipewa si chini ya dola 80 wakiwa nje ya nchi, huku wakipewa kiasi cha dola 50 wakiwa hapa nyumbani kama posho yao ya siku. Ni tofauti na kile ambacho Liuzio amekuwa akishuhudia wakipewa katika klabu yake ya sasa.

“Wanasema Timu ya Taifa ni uzalendo kwanza lakini kwa kushindwa kuwapa hata hicho kidogo nafikiri ilichangia sana kushusha morali ya wachezaji. Viongozi walikuwa wakichukua mara mbili ya kile ambacho wachezaji hupewa.Kulikuwa na vikwazo vingi kwa Nooij ndani ya timu. Kuna wakati hadi wachezaji walikuwa wakimuhurumia Nooij”

MAISHA YAKE ZAMBIA…..

Shaffih Dauda: Umekuwa mwenyeji sasa kitu gani unakipenda huko?
Liuzio; Napenda sana jinsi  ninavyoishi na wachezaji  wenzangu na majirani zangu.

Shaffih Dauda:  Vipi kuhusu chakula?
Liuzio; Mmh chakula huwa  najipikia mwenyewe.

Shaffih Dauda: Kitu gani hujakifurahi huko?
Liuzio; Tabia zao za ulevi kupita  kiasi

Shaffih Dauda: Unajiepusha vipi na hali hiyo?
Liuzio; Kutotembea ovyo.

Shaffih Dauda: Unaishi peke yako au…na klabu imekupangia?
Liuzio; Yap nipo  peke yangu, klabu imenipangia nyumba kubwa ina vyumba viwili, jiko, choo na sitting room, wadogo zangu wamekuwa wakinitembelea mara kwa mara.

Shaffih Dauda: Unafuraha kuwa huko? Kwa nini
Liuzio; Nina furaha kwa kuwa kuna baadhi ya vitu kwenye maisha vinakuwa rahisi kutokana na kipato tofauti na mwanzo.

Shaffih Dauda: Mfano…?
Liuzio; Siwezi kukaa bila kuwa na akiba kidogo bank. Tofauti na zamani nilikuwa nikaa bila kuwa na hata shilingi mia (100)

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here