Home Ligi EPL Alichosema Fabregas Kuhusu Kuongoza Mgomo Dhidi Ya Mourinho

Alichosema Fabregas Kuhusu Kuongoza Mgomo Dhidi Ya Mourinho

739
0
SHARE

Baada ya kuzuka kwa tuhuma kwamba yeye ni mmoja wa wachezaji wanaoongoza mgomo wa wachezaji wa Chelsea dhidi ya kocha wap Jose Mourinho – kiungo Cesc Fabregas ameamua kutoa yake ya moyoni juu ya shutuma hizo.

 Cesc Fabregas kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter mchana huu amekanusha taarifa zilizotolewa wikiendi iliyopita kwamba yeye ndio mchezaji aliye mbele kupinga mbinu za ufundishaji za Jose Mourinho

Kiujgo huyo umri wa miaka 28 amekanusha na mgomo baridi unaoripotiwa kuwepo Stamford Bridge na kuongeza kwamba ana mahusiano mazuri sana na mwalimu wake na amesema kuna watu wa nje ya klabu wanajaribu kutengeneza mazingira ya ugomvi ndani ya klabu.


Hatua ya kiungo huyo kuongea hadharani itatuliza hali ya sintofahamu baina ya mashabiki na wachezaji.

Hata hivyo kujitetea kwa Fabregas kutapelekea mchezaji mwingine kupewa zigo la lawama ya kuongoza mgomo ambao unatajwa sana kuwepo ndani ya timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here