Home Ligi EPL PELLEGRINI AMKINGIA KIFUA BONY

PELLEGRINI AMKINGIA KIFUA BONY

769
0
SHARE

Bony

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amewaasa mashabiki wa klabu hiyo kutoa sapoti ya kutosha kwa mshambuliaji wa timu hiyo Wilfried Bony, lakini akikiri kuwa Bony ana jambo zito sana la kuwathibitishia mashabiki juu ya ubora wake wa kuichezea klabu hiyo.

Mu-Ivory Coast huyo amefunga magoli matatu katika michezo mitano, huku akikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mshabiki, hasa hivi karubuni katika mchezo dhidi ya Norwich City baada ya kukosa nafasi nyingi za kufunga.

Lakini Pellegrini amekiri kuwa, wakati mchezaji huyo wa zamani wa Swansea City akihitajika kufanya makubwa zaidi klabuni hapo huku akiwaasa na mashabiki kutoa sapoti ya kutosha kwa mchezaji huyo.

“Pengine anahitajika kufunga, kwa sababu kwa sasa anakosa nafasi nyingi sana”, Pellegrini aliwaambia waandishi.

“Namna anaavyocheza na uwezo wake uwanjani, sio rahisi kuwa anakosa magoli namna ile nadhani anahitaji kuaminiwa”, Pellegrini aliongeza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here