Home Kimataifa LAMARCUS ALDRIDGE , SPURS WAIFANYIA KWELI CELTICS. GINOBILLI, DUNCAN, PARKER WAWEKA REKODI...

LAMARCUS ALDRIDGE , SPURS WAIFANYIA KWELI CELTICS. GINOBILLI, DUNCAN, PARKER WAWEKA REKODI YA MUDA WOTE NBA

491
0
SHARE

ALDAldridge alikuwa na pointi 24 na 14 rebounds , Kawhi Leonard aliongeza pointi 19 na Spurs kuwapiga Boston Celtics 95-87 siku ya Jumapili. ” Hakuna hakuna namna, kwa mfumo wowote atakaokutana nao itabidi ajifunze kuuzoea na kucheza nao, lazima ajifunze” Popovich alisema.

Danny Green pia anasema anajua kuwa atachukua muda kiasi kujifunza.” bado sote tunajaribu kufikiri mbali, ” Danny  alisema. “Ni bado itaendelea kuchukua muda.  Manu Ginobili alifunga pointi 13 na Boris Diaw alikuwa 10 kwa Spurs.

Aldridge alisainiwa na Spurs kwa mkataba wa miaka minne baada ya kutumikia kwa miaka tisa katika klabu ya  Portland . Kocha wa Boston Celtics  Brad Stevens amesema anadhani Spurs itakuwa kali na imara  pale Aldridge akiweza kuzoeana na kucheza vyema na wachezaji wenzake wapya.

Avery Bradley kaliongoza kwa upande wa  Boston akiwa na pointi 18 na Marcus Smart alikuwa 17. Isiah Thomas alifunga pointi 15, Jared Sullinger alikuwa na pointi 10 na rebounds nane .

Tim Duncan, Parker na Ginobili walipata ushindi wao wa 541wakiwa  pamoja , na kuipita rekodi ya  Boston iliyokuwa inashikiliwa na  Larry Bird , Kevin McHale na Robert Parish (540) kwa wachezaji watatu waliocheza pamoja katika historia ya NBA.

Kevin Mchale, Robert Parish na Larry Bird wakiwa pamoja katika benchi Boston Celtics
Kevin Mchale, Robert Parish na Larry Bird wakiwa pamoja katika benchi Boston Celtics
Manu Ginobilli, Tim Duncan na Tony Parker
Manu Ginobilli, Tim Duncan na Tony Parker

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here