Home Kimataifa KEVIN DURANT AWAKA, OKC YAENDELEA KUKITIMUA

KEVIN DURANT AWAKA, OKC YAENDELEA KUKITIMUA

490
0
SHARE

HJKevin Durant alifunga pointi 25 na kusaidia Oklahoma City Thunder kuifunga  Denver Nuggets 117-93 siku ya Jumapili usiku . Durant alipata mitupo  8 kati  ya 11 na kupata mitupo huru yote 6 na kumsaidia kocha mpya Billy Donovan kubaki hajapigwa katika NBA .

Thunders wamepata ushindi wa tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu 2011-12. Siku ya Jumapili, wachezaji saba walifunga katika tarakimu mbili mbili (double double).

Serge Ibaka alikuwa na pointi 18, rebounds 7 na blocks  5   na Westbrook alikuwa na pointi 15, rebounds 9 na kusaidia pasi 8.  Danilo Gallinari na Will Barton kila mmoja alifunga pointi 15 na Jameer Nelson aliongeza pointi 13 na pasi saba kwa Denver  Nuggets , ambayo ilipata mitupo yake kwa asilimia 38 tu.

” Robo ya tatu ni mahali ambapo sisi tulipotea na wakatuzidi, ” kocha wa Denver  Nuggets, Michael Malone alisema. “Tulikuwa ndani ya mchezo , tulikuwa tunashindana , lakini katika robo ya tatu , wao wakageuka, wakawa bora na kutushinda kwa  haraka.

” Wachezaji wote walioanza wa Oklahoma walikaa nje katika robo ya nne, na kuachia wachezaji wa akiba kuendeleza na kuendeleza uongozi na kupata ushindi.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here