Home Ligi EPL YAYA TOURE AGOMA KUBAKI UWANJANI, AKASIRISHWA NA PELLEGRINI

YAYA TOURE AGOMA KUBAKI UWANJANI, AKASIRISHWA NA PELLEGRINI

528
0
SHARE

Yaya Toure vs Pellegrini

Kweli hakuna kazi ngumu kwa kocha kama kuwa na kikosi chenye wachezaji maarufu wenye majina kama Yaya Toure. Baada ya jana Toure kuifungia goli la ushindi timu yake ya Manchester City kwa penati katika dakika ya 89 alifanyiwa sub, kitendo kilichomkasirisha na kuamua kuondoka uwanjani.

Yaya Toure alionekana kunyoosha kidole kwa jazba na ilikua ngumu kwa kocha wake Manuel Pellegrini aliyejaribu kumkumbatia lakini Toure akiwa mwenye hasira alipitiliza katika tunnel na kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Yaya Toure vs Pellegrini 2

Haijafahamika mara moja nini kiliendelea huko chumbani baada ya mchezo kati ya Toure na kocha wake Manuel Pellegrini.

Katika mchezo huo City wakiwa katika kiwango kibovu kabisa walilazimika kusubiria penati iliyosabibishwa na Raheem Sterling katika dakika ya 89 kupata goli la ushindi na kufanya matokeo kuwa 2-1 dhidi ya Norwich waliopanda daraja msimu huu.

Yaya Toure vs Pellegrini 1

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here