Home Ligi EPL MASHABIKI CHELSEA WAMBAKIZA MOURINHO

MASHABIKI CHELSEA WAMBAKIZA MOURINHO

764
0
SHARE

Mashabiki-Chelsea

Baada ya jana kukubali kichapo kingine cha bao 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Liverpool, mashabiki wa Chelsea waliamua kuimba huku wakimtaja jina kocha wao Mourinho wakati wote wa mechi.

Tajiri wa Chelsea, Roman Abramovic hakuwepo uwanjani wakati mechi hiyo iliyotajwa kuwa ya mtego kwa Mourinho lakini bila shaka aliwasikia mashabiki wakimsapoti kocha wao kupitia television nyumbani kwake.

Mourinho vs Liverpool

Baada ya mechi, pamoja na kudai hana cha kuongea huku akijibu majibu ya mkato sana, kocha Jose Mourinho alidai kwamba haondoki klabuni hapo huku akisema mashabiki hawakua vichaa kumuimba jina lake kwani wanajua jinsi yeye na wachezaji wanavyojaribu kupata matokeo.

Kwa utamaduni wa Chelsea tangu kununuliwa na tycoon Roman Abramovic, amekua akiwasikiliza zaidi mashabiki wake wanasema nini kabla ya yeye kufanya maamuzi, historia inaonesha Andres Vila Boas na Rafael Benitez walifukuzwa asubuhi baada ya jana yake kuimbiwa nyimbo za kutotakiwa na mashabiki Stamford Bridge na Abramovic akawasikiliza.

Mashabiki-Chelsea 2

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here