Home Kimataifa BAADA YA KUICHEKI UWANJANI…HII NI SUMMARY YA MECHI YA KAIZER CHIEFS VS...

BAADA YA KUICHEKI UWANJANI…HII NI SUMMARY YA MECHI YA KAIZER CHIEFS VS ORLANDO PIRATES

746
0
SHARE

870f18b9-1a7f-4a19-a10e-46f032e3f836

31 October 2o15 ndio siku ambayo mechi kati ya Kaizer Chiefs Vs Orlando Pirates imefanyika kwenye uwanja wa FNB Stadium. Mechi hii ni kubwa sana ambapo hizi ndizo club kubwa za Soweto na kuifanya kuwa moja kati ya Derby kubwa Africa.

Mchezaji wa Orlando Pirates Thabo Rakhale alionekana akiwa kwenye juhudi za kutafuta nafasi hadi ilivyofika dakika ya 16 ambapo alipiga shot on target umbali wa yard 20 lakini halikuzaa matunda.

873734e6-0ab0-45d2-98c4-bbfec6645196

Mechi ikiwa imefika dakika ya 25 goli la kwanza likangia na kuipa Orlando Pirates uongozi wa mechi kupitia mchezaji wao Issa Sarr. Ilivyofika dakika 35 Orlando walikua na nafasi ya kuongeza goli la pili lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.

Kabla timu zote hazijaenda mapumziko Kaizer wakasawazisha goli kutoka kwa Erick Mathoho na kuwaacha mashabiki wao wakiwa kwenye furaha muda wa mapumziko tofauti na wangewaacha bila goli.

9baca708-68a9-455d-97a4-4cc142f3e48c

KIPINDI CHA PILI
Kaizer walianza vizuri kipindi cha kwanza ambapo na ilipofika dakika 52 ilikua bado kidogo watupie goli la pili. Lakini dakika chache baadae Pirates waliendelea kuongoza mechi hii baada ya goli la Ayanda Gcaba dakika ya 55.

58568031-d686-49bc-8108-59e295a8c272

Mpira ukaendelea kupigwa huku Pirates wakiwa kwenye uongozi wa mechi hiyo. Dakika ya 83, Thamsanqa Gabuza akatupia goli lingine na kuwa wa mwisho kuandikwa kwenye score sheet ya mechi hiyo. Hadi mechi inaisha matokeo ni Kaizer Chiefs 1-3 Orlando Pirates

7c6e48b1-c609-4ee8-b6e3-6a8087e86d36

VIKOSI

Kaizer Chiefs: Khune, Gaxa, Mathoho, Bukenya, Masilela, Katsande, Letsholonyane, Tshabalala, Lebese, Abraw, Manqele
Orlando Pirates: Mpontshane, Nyauza, Matlaba, Sangweni, Gcaba, Sarr, Rakhale, Ntshumayelo, Gabuza, Makola, Erasmus

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here