Home Kitaifa AZAM YAREJEA KILELENI MWA VPL KWA KISHINDO

AZAM YAREJEA KILELENI MWA VPL KWA KISHINDO

515
0
SHARE
Kavumbagu (kushtoto) kishangilia kwa kucheza na Farid Musa baada ya kufunga goli la kwanza Azam ilipocheza dhidi ya JKT Ruvu

Kavumbagu (kushtoto) kishangilia kwa kucheza na Farid Musa baada ya kufunga goli la kwanza Azam ilipocheza dhidi ya JKT Ruvu

Timu ya Azam FC imerejea tena kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kufuatia ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Jana Yanga ilishikilia nafasi ya kwanza baada ya kuifunga Kagera Sugar lakini ushindi wa leo wa Azam umewarejesha tena kileleni wakifikisha jumla ya pointi 25 na kuiacha Yanga ikisalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 23.

Shomari Kapombe amefunga magoli mawili kati ya matano ambayo Azam wameshinda leo. Kapombe alifunga mabao hayo dakika ya 34 na 36 kipindi cha kwanza wakati bao la tatu lilifungwa na Kipre Tchetche dakika ya 45.

Azam walipata mabao mengine mawili kipindi cha pili, goli la nne la Azam limefungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 49 huku Kavumbagu akipiga bao la tano na kuhitimisha ushindi huo mnono wa Azam dakika ya 62.

Kitu ambacho kiliwashangaza watu wengi ni kitendo cha wachezaji wa Azam FC golikipa Aishi Manula na Jean Mugiraneza kuomba ruhusa kwa mwamuzi wa mchezo huo Anthony Kayombo ili kwenda kujisaidia kwa nyakati mbili  tofauti.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here