Home Kitaifa AJIB: KILA MSIMU NAWEKA HAT-TRICK

AJIB: KILA MSIMU NAWEKA HAT-TRICK

532
0
SHARE
Ibrahim Ajib amesema kila msimu anataka kupiga hat-trick
Ibrahim Ajib amesema kila msimu anataka kupiga hat-trick

Straika wa Simba Ibrahim Ajib amesema anafurahi kufunga hat-trick na kila msimu atakua akifafanya hivyo pindi akipata nafasi. Ajib amesema awali washambuliaji wa Simba walikuwa wakishindwa kufunga magoli ukilinganisha na nafasi ambazo zinatengenezwa lakini mwalimu amelishughulikia tatizo hilo ndio maana jana wameweza kufunga idadi kubwa ya magoli.

“Mchezo ulikuwa mzuri nafurahi tumeshinda kwa magoli mengi lakini nafurahi pia kufunga magoli matatu (hat-trick)”.

“Tumeweza kufunga magoli mengi kwasababu tulijua tatizo letu la kupoteza nafasi nyingi, mwalimu kalifanyia kazi ndiomaana tumeweza kupata ushindi mkubwa”, alisema Ajib ambaye jana alikuwa kwenye mwonekano mpya baada ya kukata nywele ambazo alionekana nazo msimu uliopita na mechi kadhaa zilizopita za msimu huu.

Alipoulizwa mashabiki wa Simba watarajie nini kutoka kwake kwasababu amekua hapati nafasi ya kucheza kwenye mechi nyingi ambazo Simba imeshacheza, alijibu: “Kila msimu naweka hat-trick”.

Ajib ameshafunga hat-trick tatu akiwa na Simba, hat-trick yake ya kwanza ilikuwa wakati klabu hiyo ikicheza michuano ya Mapinduzi Cup visiwani Zanzibar mapema mwaka huu. Alipiga hat-trick ya pili kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu uliopita kisha ya tatu lakini ikiwa yapili kwenye VPL ilikua ni jana dhidi ya Majimaji.

Kijana huyo ambaye ni chipukizi alionesha kiwango kizuri msimu uliopita lakini msimu huu amekumbana na wakati mgumu hasa kocha wa timu hiyo Dylan Kerr anapoamua kumchezesha mshambuliaji mmoja ambapo nafasi hiyo huangukia kwa Hamisi Kiiza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here