Home Kitaifa SAMATTA AISOGEZA TP MAZEMBE KWENYE UBINGWA WA AFRIKA

SAMATTA AISOGEZA TP MAZEMBE KWENYE UBINGWA WA AFRIKA

715
0
SHARE

USM vs TP Mazembe

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anaekipiga kwenye timu ya TP Mazembe ya Congo DR usiku wa Jumamosi November 1 kuamkia Jumapili aliisaidia klabu yake kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya USM Alger ugenini wakati wa mchezo wa kwanza wa fainali ya klabu bingwa Afrika (Africa Champions League) uliochezwa kwenye kwenye uwanja wa Omar Hamad, Algiers nchini Algeria.

Kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Zambia Rainford Kalaba alianza kuifungia Mazembe goli la kwanza dakika ya 27 kipindi cha kwanza kwa shuti kali akiwa zaidi ya umbali wa mita 25 kutoka golini.

Lakini dakika chache baadaye, Kalaba alipata kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga mchezaji wa USM na kupelekea Mazembe kucheza wakiwa pungufu kwa muda wote uliosalia kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili TP Mazembe walipata mkwaju mwingine wa penati baada ya mchezaji wa USM kuushika mpira kwa makusudi akiwa kwenye eneo la hatari na kumzuia Samatta kufunga. Mwamuzi wa mchezo huo Gehad Grisha kutoka Misri alimtoa mchezaji huyo kwa kadi nyekundu.

TP Mazembe fans

Hata hivyo golikipa wa USM Alger alidaka mkwaju huo wa penati uliopigwa na kuinyima Mazembe goli la pili.

Samatta aliifungia timu yake goli la pili dakika ya 79 kwa penati kufuatia yeye mwenyewe (Samatta) kuangushwa kwenye eneo la hatari wakati alipomtoka beki wa USM na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo iliwekwa wavuni na Samatta.

USM Alger walipata bao lao la kufutia machozi dakika ya 88 kipindi cha pili na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Mazembe kuondoka wakiwa kifua mbele kwa goli 2-1.

Ushindi huo wa ugenini unaiweka TP Mazembe kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Afrika ngazi ya vilabu wakiwa wanasubiri mechi ya marejeano itakayochezwa November 8, 2015 wakati TP Mazembe watakapokuwa wenyeji wa mchezo huo jijini Lubumbashi.

Nyota mwingine wa Tanzania Thomas Ulimwengu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha TP Mazembe kilichoanza kwenye mchezo huo na kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa kuwapa wakati mgumu walinzi wa USM hali iliyopelekea wamchezee rafu kila mara.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here