Home Kimataifa OKC CHUPUCHUPU, YAICHAPA ORLANDO MAGIC

OKC CHUPUCHUPU, YAICHAPA ORLANDO MAGIC

467
0
SHARE

thuRussell Westbrook na Kevin Durant wamefikisha mengi makubwa na yanayovutia ambayo mara nyingi yamekuwa  mambo ya muhimu kwa klabu yao ya Oklahoma City Thunder katika  NBA. Mojawapo ni kazi waliyoionyesha usiku wa kuamkia leo katika mechi dhidi ya Orlando Magic.

Westbrook alifunga point 48, pasi 8 na Rebound 11 ikiwemo point 3 ya muhimu kabisa katika dakika za mwisho za muda wa kawaida. Durant alifunga point 43 na kudaka rebound 12 katika ushindi wa 139-136 ambao ulipatikana baada ya kuongezwa kwa dakika mara mbili mfulululizo. (two overtimes )

” Walicheza mchezo mgumu sana na walitumia nguvu hasa. Sisi tulibahatika kurejea mchezoni katika kipindi cha pili na kudhibiti mchezo, ” Durant alisema. “Mchezo huu umenisaidia sana .

Tobias Harris aliingoza Magic kwa pointi 30 . Nik Vucevic aliongeza 26, na Victor Oladipo alikuwa na  pointi 21, 13 rebounds na pasi  10 (Triple Double)

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here