Home Kimataifa HALI YA LAMAR ODOM YAIMARIKA, KHLOE KARDASHIAN NA JAMES HARDEN KATIKA SINTOFAHAMU

HALI YA LAMAR ODOM YAIMARIKA, KHLOE KARDASHIAN NA JAMES HARDEN KATIKA SINTOFAHAMU

506
0
SHARE
khloe kardashiana akiwa na Lamar Odom
Lamar Odom
Lamar Odom

Miujiza kutokea , na pengine  Lamar Odom anapokea miujiza hiyo. Khali ya Lamar Odom imekuwa na unafuu ghafla hasa baada ya madaktari kuthibitisha kuwa hatohitaji tena kupandikizwa Figo kama ambavyo awali ilidhaniwa.

Chanzo kimeeleza  kwamba hali ya Odom ina ahuni kwa kaisi kikubwa na imeboreka baada ya awali kuripotiwa kuwa mchezaji wa zamani wa NBA , Lamar Odom 35, alikuwa anasumbuliwa na figo kushindwa mwishoni kufanya kazi mpaka mwishoni mwa wiki hii iliyopita.

Alikuwa aalikuwa anafanyiwa usafishaji damu na figo (dialysis) , ambayo ilikuwa ikifanywa kwa takribani masaa 6 kwa siku, na alikuwa katika haja ya kuhitaji kupandikiza figo.

Odom amepata mabadiliko ya kiafya ya ghafla na ya kushangaza  huku ikisemekana  matibabu yake yangeweza kuchukua muda mrefu sana. Na Taarifa zilizopo ni kwamba Lamar Odom kwa sasa anaweza kutembea kwa msaada.

Ikumbukwe iliripotiwa awali kuwa Lamar alipata Stroke (kupooza kwa baadhi ya viungo) na ubongo kuathirika.

Aidha iliripotiwa kuwa Khloe Kardashian pamoja na kuondoa hati ya talaka mahakamani hakuwa na mpango wa kmrudia Lamar Odom, bali alifanya hivyo ili kujaribu kusaidia katika kuiweka khali yake kiafya katika mlengo sahihi.

Na taarifa za ndani zinasema alipanda ndege ya kukodi jumatano kuelekea katika mechi ya Houston. Kikubwa ilidaiwa safari yake ilikusudia  kumuona mpenzi wake wa sasa James Harden ambaye alikuwa mchezaji bora wa pili wa msimu uliomalizika nyuma ya Stephen Curry.

James Harden
James Harden

Lakini swali ni kama wataweza kuishi pamoja endapo Lamar atapona, kwani Khloe ameonekana mara kadhaa akikiri kuwa ana upendo wa dhati kwa Lamar Odom. Kitu kingine ni uwezekano wa kuwa na kipindi kinachouza zaidi kama Lamar Odom akipona kwani watu watataka kuona masiha yake baada ya madawa.

khloe kardashiana akiwa na Lamar Odom
khloe kardashiana akiwa na Lamar Odom

TUSUBIRI

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here