Home Kimataifa MAADUI MARK CUBAN NA DEANDRE WAKUTANA, CLIPPERS IKIMUUA MAVERICKS

MAADUI MARK CUBAN NA DEANDRE WAKUTANA, CLIPPERS IKIMUUA MAVERICKS

500
0
SHARE

njUlikuwa usiku wa kufurahisha kutokana na mahasimu wa ghafla kukutana sehemu moja. Wakati wa maandalizi ya msimu mpya mmiliki wa klabu ya Dalls Mavericks Mark Cuban aliamini kuwa ameshapata saini ya mchezaji Deandre Jordan kutoka Los Angeles Clippers. Dallas ikishinda 104-88.

Lakini mambo yalibadilika mwishoni baada ya Deandre kushawishiwa na inavyosemekana Chris Paul na Blake Griffin na kuvunja makubaliano ambayo yalionekana kuwa mkataba wa awali.

Pengine faraja kubwa katika mchezo huu ni yeye kubaki katika klabu yake na kupata ushindi dhidi ya klabu ambayo ni wazi inamchukia kwa sasa.

Mark Cuban alikuwepo uwanjani alfajiri ya leo pale Staple Center na hakusita kusema kuwa “Deandre ndo nani, ninachofahamu ni kuwa Clippers wana centre mzuri na bora”. Akaenda mbali zaidi na kusema “Clippers ni walewale, hata wabadili wachezaji, wamebaki kuwa walewale kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30”.

Blake Griffin alikuwa na pointi 26 na 10 rebounds , na Jamal Crawford aliongeza pointi 15 kwa  Clippers  katika ushindi wa 104-88 dhidi ya Dallas Mavericks Alhamisi usiku kule  Los Angeles katika mechi ya ufunguzi nyumbani kwa clippers pale Staples Center (wanatumia uwanja mmoja na Lakers).

Jordan alikuwa na pointi sita , 15 rebounds na kuzuia  mitupo 4 ya Mavericks katika mechi yake ya kwanza dhidi ya klabu hiyo iliyoamini ilikuwa imekwishamsajili. Austin Rivers akaongeza point 14 kwa klabu hiyo inayofundishwa na baba yake Doc Rivers.

Dirk Nowitzki alifunga pointi 16 kwa Mavericks , ambayo  ilicheza bila kuwa na wachezaji wake muhimu Deron Williams na Wesley Matthews.

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here