Home Kimataifa KNICKS WAANGUKIA PUA KWA MWEWE WA ATLANTA

KNICKS WAANGUKIA PUA KWA MWEWE WA ATLANTA

564
0
SHARE

knWalau sasa Atlanta Hawks unaweza kuwaita mwewe hawa walipata ushindi wao wa kwanza baada ya kupoteza mchezo wa awali na hatimaye tulishuhudia ile njaa ya msimu uliomalizika na fomu iliyowafanya kuongoza kanda ya Mashariki.

Point guard Jeff Teague alifunga pointi 23, Al Horford aliongeza 21 na Hawks ikawachapa New York Knicks 112-101 Alhamisi usiku wa kuamkia leo ijumaa na kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu. Kyle Korver alikuwa na pointi 15 na Millsap aliongeza pointi 11 na 11 rebounds kwa Atlanta.

“Tunajaribu kurejea katika ubora wetu ambao ulizoeleka”,Paul Millsap alisema. “Tulicheza vizuri usiku wa leo, ” kocha Mike Budenholzer alisema. “Nadhani kundi la kwanza lilianza vyemma na kutuweka mahala sahihi katika robo ya kwanza . ”

Carmelo Anthony alifunga pointi 25.  Robin Lopez yeye akamaliza na pointi 8 pekee kwa klabu ya New York Knicks. Kristaps Porzingis alimaliza na pointi 10 na rebound 8.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here