Home Kitaifa KAMATI YA MUDA YA ZFA YAPOKEA KWA MIKONO MIWILI BARUA YA CAF

KAMATI YA MUDA YA ZFA YAPOKEA KWA MIKONO MIWILI BARUA YA CAF

518
0
SHARE
Hussein Ali Ahmada mwenyekiti wa muda wa kamati inayosimamia soka la Zanzibar
Hussein Ali Ahmada mwenyekiti wa muda wa kamati inayosimamia soka la Zanzibar
Hussein Ali Ahmada mwenyekiti wa muda wa kamati inayosimamia soka la Zanzibar

Na.  Abubakar Kisandu

Mwenyekiti wa kamati ya muda inayosimamia soka hapa visiwani Hussein Ali Ahmada amesema wanalishukuru sana Shirikisho la kandanda Afrika (CAF) baada ya kuwapelekea barua wao na hiyo inaonesha kwamba kamati yao inatambuliwa.

“Tunawashukuru sana CAF kututaka sisi kamati kufanya hiyo kazi na hii inaonesha kuwa sisi tunatambulika kote huko”, amesema Hussein.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa wanatarajia kufanya jitihada zote kuondosha soka mahakamani kama walivvotakiwa na shirikisho hilo.

“Tutajitahidi kuendelea kuondosha hizo kesi mahakamani lakini hawa waliopeleka barua huko CAF ndio waliokuwa wanataka soka la Zanzibar lisichezwe”.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jana iliitaka Kamati ya muda inayoongoza Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) iondoe mahakamani mashtaka yote dhidi ya uongozi halali wa ZFA.

CAF imesisitiza kuwa kwa mujibu wa katiba yao na FIFA ni marufuku masuala ya mpira kupelekwa mahakamani, ZFA ni mwanachama mshiriki wa CAF (Associate Member).

Katika barua yao hiyo ya jana CAF inawahimiza kamati ya muda ya ZFA hadi tarehe 07 Novemba, 2015 iwe imetekeleza maagizo na kuhakikisha uongozi halali uliochaguliwa na ZFA unarejea katika shughuli zake uongozi ZFA.

Jambo hilo lisipotekelezwa CAF imesema itaifungia Zanzibar uanachama wake. Kikanuni na kikatiba kufungiwa uanachama maana yake ni mwanachama husika kusitishwa ushiriki katika shughuli zote zinazosimamiwa na FIFA, CAF na wanachama wake wote.

Shughuli hizo ni pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa, kozi mbalimbali na misaada ya kifedha, vifaa, ufundi nk.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here