Home Kitaifa ‘HIVI NDIVYO VPL INAVYOKUWA NA USHINDANI UDHAIFU’

‘HIVI NDIVYO VPL INAVYOKUWA NA USHINDANI UDHAIFU’

576
0
SHARE

YANGA BINGWA

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

‘Dakika 90 ni kama vita ndani ya uwanja, vita ya wachezaji 22 kila mmoja akitaka kuhakikisha timu yake inapata ushindi. Lakini baada ya michezo 135 kuchezwa na magoli 113 kufungwa kufikia mechi za Alhamisi, malalamiko kuhusu waamuzi ni ya kiwango cha juu. Ni ngumu kwa klabu kupata ushindi katika uwanja wa ugenini hata kama itakuwa na uwezo.

Uchumi dhaifu, Mtibwa, Toto, Coastal, Tanzania Prisons

Klabu kulalamikia ukata zikiwa katika mzunguko wa tano tu kwa kiasi kikubwa pia husababisha kupunguza ushindani wa kweli katika ligi kuu ya bara. Licha ya mechi nyingi kuonekana ngumu lakini ni timu chache sana zenye uwezo wa kucheza mchezo wa nguvu kwa walau dakika 70.

Klabu kama Toto Africans ya Mwanza inaweza kuleta ushindani mkubwa msimu huu lakini matatizo ya pesa yanachangia kupunguza ari yao, nguvu na utimamu wa kimwili na kiakili.

Africans Sports, Coastal Union ni klabu nyingine ambazo zinashindwa kucheza vizuri katika ligi kwa sababu za kipesa. Wachezaji wa klabu hizo wanadai baadhi ya mishahara na hela zao za usajili. Coastal licha ya kufunga goli moja tu katika gemu 9 msimu huu bado huwezi kuwahukumu kwamba ni timu mbovu.

Wanacheza lakini kwa sababu ya kukamilisha ratiba tu ila kwa ‘lugha yao ya mwili’ ni timu ambayo haijajipanga vizuri kiutawala. Wamebaki kutegemea udhamini wa Vodacom na AzamTv wakati kiukweli udhamini huo hauwezi kukidhi mahitaji yote muhimu.

Toto licha ya kuandamwa na ‘ukata mkubwa’ kiasi cha kupelekea kujiuzulu kazi kwa mkufunzi wao mkuu, MjerumaniMartin Grelics, timu hiyo imekuwa na matokeo mazuri. Katika gemu nne za ugenini wameshindwa mara mbili na kuambulia sare mbili. Imeshinda gemu 3 kati ya 9 ilizocheza lakini ndiyo timu yenye matatizo zaidi ya kipesa katika VPL.

Klabu kama Toto, Sports, Coastal, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, JKT Mgambo, Tanzania Prisons, Majimaji FC, Ndanda FC zinatakiwa kutafuta wadhamini ili kukabiliana na mazingira ya sasa ya ligi. Wachezaji wapate stahiki zinazostahili. Viongo wa klabu wakiwajibika katika hili watafanikiwa.

Stand United ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita kwa sababu ya ukata lakini sasa wana udhamini wa zaidi ya bilioni mbili. Wamepambana kuhakikisha wanafanya ushawishi kwa kampuni iliyopo mkoani kwao Shinyanga na kufanikiwa sasa wanacheza ligi kwa lengo la kushinda ubingwa au kumaliza katika nafasi ya kuiwakilisha nchi.

Toto imepoteza mkufunzi makini sana, ni wao wenyewe walio athiri ufanisi wa kocha wao kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri zaidi. Grelics amesema ni suala la kuvunja moyo kuwaona wachezaji wake wakishindwa kujikidhi kimaisha kwa ukosefu wa mishahara huku wakishindwa kufanya mazoezi mara kadhaa kwa sababu ya kushinikiza malipo yao ya usajili na mishahara, ukosefu huo wa hela za maandalizi umekuwa ukishusha viwango vya wachezaji. Matatizo kama haya yakishughulikiwa Tanzania bara inaweza kutengeneza moja ya ligi bora Afrika, hakika.

Nje ya Vodacom  na  AzamTV, Yanga, Azam, Simba, Stand na Mbeya City hazitoshi.

Tunaposema ligi ina ushindani ni kwa sababu baadhi ya mechi zinachezeshwa kwa usawa na inapotokea mechi zinazohusisha klabu zenye uchumi wa kushabihiana tegemea mechi ngumu sana. Yanga SC wamesimamishwa na Mwadui FC kwa sare ya 2-2. Mwadui FC inakusanya wachezaji ‘mastaa wazawa’ wenye uzoefu. Wako vizuri kiuchumi ndiyo maana wameweza kuwasaini wachezaji wa darasja la juu nchini. Wako timamu kimwili na kiakili.

Mbeya City, Stand United, Azam FC, Yanga SC kwa sasa naweza kusema ni timu hizi tu zenye udhamini wa kuweza kuwasaidia kucheza ligi katika ushindani kuanzia mwanzo wa msimu hadi mwisho. Si rahisi kupata ligi bora wakati ni klabu tano tu zenye uwezo wa kumudu mahitaji muhimu ya wachezaji na timu kiujumla. Klabu zisizo na udhamini binafsi ni vyema zikapambana kuhakikisha wanapata wadhamini kama kweli wanataka kucheza ligi kwa kiwango cha ushindani.

Waamuzi ‘Vimeo’

Waamuzi huwa wanaharibu mechi, tazama marudio ya gemu ya Azam FC 1-1 Yanga SC, ni mwamuzi tu aliyetaka kubalidi matokeo ambayo yalistahili kupatikana katika mechi hiyo. ‘Aliwapa Yanga kiki ya penati isivyo halali’.

Sijui huwa ni rushwa kama alivyodai mkufunzi wa Azam FC, Stewart Hall au ni mapenzi binafsi ya waamuzi kuingilia matokeo. Waamuzi ni tatizo pia kwa sababu wanashindwa kuwa ‘fair’ kwa baadhi ya timu.

Huwezi kuwa na ligi bora wakati waamuzi wanaamua matokeo kila siku. TFF iliwapunguza kwa asilimia kubwa kwa kudhani kuwa kufanya hivyo kutapelekea hawa wachache walio salia katika VPL kuchezesha kwa haki. Lakini imekuwa mbaya zaidi tena ligi ikiwa ni ‘mbichi’ kabisa.

Bakari Shine, mkufunzi mkuu wa Mgambo JKT amelalamikia penati ambayo Toto Africans walipata katika gemu yao ya juzi katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Shime amesema mwamuzi aliamua kuwapa ushindi wenyeji kwa kuwa penati hiyo haikuwa sahihi. Licha ya kuongezewa posho, wengine kukatwa lakini waamuzi wetu wameendelea kuvurunda kwa sababu gani?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here