Home Ligi EPL Hili ndio dau walilotoa kampuni ya kichina kuinunua Man United

Hili ndio dau walilotoa kampuni ya kichina kuinunua Man United

617
0
SHARE

Kama ulikuwa unahitaji uthibitisho mwingine juu ya ukubwa wa ligi kuu ya England na klabu ya Manchester United katika ulimwengu wa soka basi story hii itakupa picha halisi.


Kuna taarifa kutoka Mashariki ya Mbali kwamba kuna kampuni imetoa ofa ya 3.5 billion euro kwa ajili ya kununua hisa kwenye klabu hiyo ya jiji la Manchester. 3.5 billion kwa ajili ya manunuzi ya hisa.

Gazeti linaloheshimika la kichina liitwalo Titan limeripoti Ijumaa hii.

Ripoti ya Titan inasema wawekezaji wa kampuni hiyo wameshawasiliana na Manchester United. Msemaji wa kampuni ya CITIC Capital, ambao wametajwa kuhusika na ofa hiyo kwenda kwa United – amekanusha kampuni yake kuhusika na ofa hiyo.

Kwa upande wa familia ya Glazer, wenyewe wamegoma kuuza hisa zao za Class B japo kwa dau lilotajwa inaaminika watakuwa tayari kuuza sehemu ya klabu.

Wawekezaji wa kichina ambao pia wanamiliki Atletico Madrid kwa 20% na kampuni ya CITIC wameripotiwa na gazeti la Titan kwamba wameanza kuandaa mechi za kirafiki wakati wa Pre Season huko China ili kuweza kuwavutia Glazers kuuza timu yao.

 Wiki iliyopita, Raisi wa China XI Jinping alisisitiza wafanyabiashara wa nchi hiyo kuweka mazingira ya kihusiano wa michezo kati ya nchi yake na Uingereza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here