Home Kitaifa DONALD NGOMA ANAWEZA KUVUNJA REKODI YA AMIS TAMBWE VPL?

DONALD NGOMA ANAWEZA KUVUNJA REKODI YA AMIS TAMBWE VPL?

788
0
SHARE

DON


NA Baraka Mbolermbole, Dar es Salaam

Msimu wa 2013/14 mshambulizi raia wa Burundi, Amis Tambwe alifanikiwa kuvunja rekodi ya ufungaji katila ligi kuu Tanzania Bara kwa wachezaji raia wa kigeni. Mkenya, Boniface Ambani alikuwa akishikilia rekodi ya mfungaji wa magoli mengi zaidi kwa msimu. Ambani akiwa katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, 2008/09 alifunga jumla ya magoli 18 kabla ya Tambwe kufunga mara 19 na kuvunja rekodi hiyo akiwa na klabu ya Simba SC.

Mfungaji bora wa kigeni aliyefunga magoli machache zaidi kwa msimu ni Mganda, Michael Katende ambaye alifunga magoli yasiyozidi 12 msimu wa 2007/08 akiwa na klabu ya Kagera Sugar. Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast yeye alishinda tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2012/13 akiwa na mabao 14 kwa maana hiyo hakuna mchezaji ‘ proo’ aliyefunga mara nyingi kwa msimu kama Tambwe katika ligi kuu ya bara.

Wachezaji wawili wa Azam FC ( Kipre na Mrundi Didier Kavumbagu) tayari wamefunga zaidi ya magoli 80 kati ya mwaka 2011 hadi sasa na hadi kufikia michezo ya raundi ya Tisa msimu huu wachezaji wa kigeni wameonekana kuwa hatari zaidi katika ufungaji.

Mshambulizi na kinara wa mabao katika klabu ya Simba, Mganda, Hamis Kiiza alifunga goli lake la sita katika mchezo wan ne upande wake wakati Simba iliposhinda 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katikati ya wiki hii. Kiiza ndiye mchezaji mwenye takwimu nzuri zaidi msimu huu katika ufungaji. Amekuwa msaada mkubwa sana kwa timu yake kwani amefunga mabao 6 kati ya 9 ya timu yake katika gemu 8 ilizokwisha cheza.

Tambwe ameendelea kufanya vizuri. Msimu uliopita alifunga mara 15 na tayari amefunga mara tano msimu huu. Kipre pia amefunga mara nne lakini mtu ambaye anaweza kufikia rekodi ya Tambwe na kuivunja na mshambulizi wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, Donald Ngoma ambaye kasi yake kwa hakika inawatisha walinzi na walimu wengi wa timu pinzani msimu huu.

Ikiwa ndiyo kwanza amecheza mechi 8 za ligi kuu ya Tanzania Bara tangu aliposajiliwa kutoka FC Platimun ya Zimbabwe, Ngoma alifunga magoli mawili na kuisaidia timu yake kupata sare ya kufungana 2-2 na Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga katikati ya wiki hii. Magoli hayo mawili yamemfanya kufikisha jumla ya magoli 7.

Amekuwa akicheza kwa nguvu sana, kasi pale anapovamia goli la wapinzani wake. Uchezaji wake wa nguvu umemfanya kuweza kuwamudu walinzi wengi aliokutana nao. Amekuwa akiwekewa ulinzi mkali katika kila mechi lakini amejitahidi kucheza kwa nidhamu. Alifunga katika mechi ngumu dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika gemu ambayo alikabwa sana na mlinzi wa Taifa Stars, Salim Mbonde.

Mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Coastal na alifanikiwa kufunga, akafunga tena katika gemu dhidi ya Tanzania Prisons, JKT Ruvu na Toto Africans. Je, ataweza kufikia rekodi ya Tambwe ya kuwa mfungaji bora mgeni alifunga idadi kubwa zaidi ya magoli kwa msimu?. Yanga itacheza na Kagera Sugar Jumamosi hii katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora…..

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here