Home Kimataifa OKLAHOMA CITY THUNDER YAWANYOOSHA SAN ANTONIO SPURS

OKLAHOMA CITY THUNDER YAWANYOOSHA SAN ANTONIO SPURS

538
0
SHARE
Russell Westbrook akikabwa na Tony Parker

 

Russell Westbrook akikabwa na Tony Parker
Russell Westbrook akikabwa na Tony Parker

Capture

Wakiwa wanamkaribisha tena uwanjani mchezaji wao bora Kevin Durant, na pia wakicheza kwa mara ya kwanza mechi yao ya ushindani chini ya Billy Donovan kocha wao mpya huyu.

Klabu ya Oklahoma City Thunder alfajiri ya leo ilipata matokeo chanya baada ya kuishinda timu ngumu ya San Antonio Spurs kwa vikapu 112-106.

Staa wa mchezo huo alikuwa ni Russell Westbrook aliyeifungia timu yake point 33 na kutoa assist 10. Mchezaji Durant akianza kwa tabu kwa kukosa vikapu vyake vya mwanzo lakini alifanikiwa kumaliza na point 22 katika mchezo huo.

Enes Kanter alishinda Point 15 na kudaka rebound 16 akitokea benchi, jambo ambalo linaweza kuwa silaha kubwa kwao msimu huu.

San Antonio walikuwa wanaongoza kwa tofauti ya Point 7 mpaka robo ya mwisho, na Kawhi Leonard akifunga point 32, ambazo ni nyingi zaidi katika maisha yake ya kikapu kuwahi kuzifunga.

LaMarcus Aldridge mchezaji wao mpya yeye alimaliza na point 11 pekee na kudaka rebound 5 katika mechi yake ya kwanza baada ya miaka 9 na  Portland Trail Blazers.

Manu Ginobilialifunga point 11 na Tony Parker akaongeza  10 kwa San Antonio.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here