Home Kitaifa EXCLUSIVE INTERVIEW: NIMEFURAHI KUITWA STARS, LAKINI SIIFAHAMU ALGERIA YA SASA-MAGULI

EXCLUSIVE INTERVIEW: NIMEFURAHI KUITWA STARS, LAKINI SIIFAHAMU ALGERIA YA SASA-MAGULI

552
0
SHARE
Elius Maguli, mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Stand United ya Shinyanga
Elius Maguli, mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Stand United ya Shinyanga
Elius Maguli, mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Stand United ya Shinyanga ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Stand United, Elius Maguli ameitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ ikiwa ni miaka miwili tangu alipoiwakilisha kwa mara ya mwisho miaka miwili iliyopita. Maguli alikuwa na msimu mgumu katika klabu ya Simba mwaka uliopita ameanza msimu huu kwa kasi kubwa. Amefunga magoli nane katika gemu tisa alizoichezea klabu yake mpya ya mjini Shinyanga.

“Ni mwanzo mzuri kwangu, namshukuru Mungu kwa kuanza vizuri msimu, hii ni dalili njema. Nashukuru Mungu nimerejea katika timu ya Taifa, ni miaka miwili sasa nilikuwa nje ya timu hiyo kwa kweli nimefurahi sana kuitwa kwa mara nyingine”, anasema Maguli wakati nilipofanya naye mahojiano baada ya kutangazwa kwa kikosi cha Stars ambacho kitaivaa ‘timu namba moja kwa ubora’ Afrika, timu ya Taifa ya Algeria.

“Kwa kipndi hiki kifupi sijaweza kuifahamu Algeria ya sasa ipo vipi ,lakini kama kutakua na habari ya kuifahamu kwaajili ya kuikabili nafikiri tunaweza kutazama baadhi ya video zao ili tuone wako vipi. Kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri. Siifahamu Algeria ila kwa muda uliopo nitaendelea kutazama baadhi ya mechi zao”.

Kocha wa Stars, Charles Mkwassa amewarejesha Jonas Mkude, Salum Abubakar, Salim Mbonde na Maguli huku akiwaita kwa mara ya kwanza Hassan Kessy na Malimi Busungu.

Maguli amekataa katakata kuzungumzia ‘msimu wake mgumu’ akiwa Simba kwa madai kuwa amefungua ukurasa  mpya katika maisha yake ya mpira. Maguli alifunga magoli matatu tu katika ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita akiwa mchezaji wa Simba, alitemwa na kocha Muingereza, Dylan Kerr wakati wa usajili uliopita kwa madai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Ruvu Shooting anapoteza sana nafasi za kufunga.

“Ukweli kwa sasa sipendi kuzungumzia habari za Simba,  sababu nimefungua ukurasa mpya,  ni sawa na mpangaji anapohama katika nyumba ya kupanga, sidhani kama anaweza kuwa bado akizungumzia habari ya nyumba ile, badala yake anaangalia ya pale alipo”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here