Home Kimataifa NEW YORK KNICKS YAIFUMUA MILWAUKEE BUCKS

NEW YORK KNICKS YAIFUMUA MILWAUKEE BUCKS

481
0
SHARE

BGDerrick Williams alifunga pointi 24 na kinda  mwenye umri wa miaka 20, Kristaps Porzingis alikuwa 16 katika mechi yake ya kwanza ya NBA , na hivyo kusababisha New York kuichapa Milwaukee Bucks  122-97 siku ya Jumatano usiku katika mechi ya ufunguzi wa msimu kwa kila timu.

Knicks ina matumaini kuwa orodha ya majina mapya yanayomzunguka Carmelo Anthony itawasaidia kurejea katika ubora wao kutoka katika historia mbaya kabisa ya kupoteza michezo 65 kwa  msimu wa mwaka jana.

Kwa usiku mmoja angalau, walianza kwa kupata ushindi dhidi ya timu inayopewa nafasi ya kuibuka msimu huu na kufanya vyema ya Milwaukee Bucks.

Greg Monroe aliongoza Bucks kwa kufunga pointi 22 na kudaka rebound 14 . Kocha Jason Kidd hakusita kumsifia kuwa kafanya vyema sana katika mchezo huo.

Jabari Parker na Giannis Antetokounmpo walikosekana katika mchezo huo kwa upande wa Bucks. Jabari Parker anauguza majeraha ya goti huku Giannis yeye akiwa na adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here