Home Kitaifa MGOSI: KAZI YANGU NI KUHAKIKISHA SIMBA INAPATA USHINDI

MGOSI: KAZI YANGU NI KUHAKIKISHA SIMBA INAPATA USHINDI

623
0
SHARE
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi

Mshambuliaji mkongwe na nahodha wa Simba Mussa Hassan Mgosi aliingia kipindi cha pili akitoka kwenye benchi kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza wakati Simba ikicheza dhidi ya Coastal Union mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.

Baada ya Mgosi kuingia, alipata nafasi kadhaa za kufunga lakini alishindwa kuipatia Simba goli kutokana na nafasi zilizotengenezwa na timu yake.

Mtandao huu ulifanya mahojiano mafupi na Mgosi baada ya kumalizika kwa mchezo huo  kutaka kujua kama kuna tatizo lolote kwa nyota huyo aliyefanya vizuri akiwa na Mtibwa Sugar msimu uliopita hali iliyoushawishi uongozi wa Simba kumrejesha Msimbazi.

Mgosi amesema yeye anacheza kuisaidia timu ipate ushindi bila kujali nani kafunga au atafunga na kama itatokea akapata nafasi ya kufunga basi atafanya hivyo.

Simba vs Coastal 2“Yani watu wanavyonichukulia mimi ni tofauti na nilivyo, mimi sio lazima nifunge, ninachokiangalia mimi ni kufanikisha timu yangu ipate ushindi. Siwezi kucheza mpira kama Mussa Mgosi basi nitoke na mpira katikati niende kufunga, kama nikipata nafasi ya kufunga nitafunga”, amesema Mgosi.

Mgosi bado hjafunga goli tangu kuanza kwa ligi msimu huu licha ya kupata nafasi mara kadhaa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba. Hamisi Kiiza ndiye mshambuliaji wa Simba anaeongoza kwa kufunga hadi sasa akiwa ameshafunga magoli sita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here