Home Kitaifa MAYANJA AWAMWAGIA PONGEZI WAAMUZI LICHA YA KIPIGO

MAYANJA AWAMWAGIA PONGEZI WAAMUZI LICHA YA KIPIGO

761
0
SHARE
Mwamuzi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union Jonesia Rukya akimuonesha kadi ya njano mchezaji wa Coastal Union kwa kumchezea vibaya Ramadhani Kessy

Kocha mkuu wa timu ya Coastal Union Jackson Mayanja ameibuka na kuwamwagia sifa waamuzi waliochezesha mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union akisema wamecheza mchezo huo kwa kiwango cha juu.

“Waamuzi leo (jana) wamechezesha mpira vizuri sana, wote watatu nimeona wamechezesha kwa kiwango cha juu sana. Waamuzi hawa wapo kwenye ‘level’ ya juu” Mayanja aliwasifu waamuzi japo mara kadhaa mashabiki wa Simba walikuwa wakipiga kelele kuashiria kutokubaliana na maamuzi ya waamuzi hao.

Hali hiyo imekuwa ni tofauti na makocha wa timu nyingine nyingi zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa makocha kuwapongeza waamuzi hasa pale timu zao zinapokuwa zimepoteza mchezo. Makocha wengi wamekuwa wakisikika wakiwapongeza waamuzi pale timu zao zinapoibuka na ushindi, kinyume na hapo waamuzi wamekuwa wakitupiwa mizigo ya lawama na makocha.

Mara nyingi makocha wamekuwa wakikwepa kubeba lawama pindi timu zao zinapofungwa na badala yake huwababesha lawama waamuzi kwamba ndio waliosababisha timu zao kufungwa.

Waamuzi waliochezesha mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union walikuwa wanaongozwa na mwamuzi wa kati Jonesia Rukya (Kagera), mshika kibendera namba moja John Kanyenye (Mbeya), mshika kibendera namba mbili Grace Wamara (Kagera) na fourth official Omar Kambangwa (Dar es Salaam).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here