Home Kimataifa KOBE AREJEA, LAKERS YAKALISHWA

KOBE AREJEA, LAKERS YAKALISHWA

526
0
SHARE
Kobe akijaribu kufunga
Kobe akijaribu kufunga
Kobe akijaribu kufunga

Ricky Rubio alikuwa na kazi ya juu kwa kufunga pointi nyingi zaidi katika maisha yake.

Alifunga  pointi 28 na pasi 14 na Timberwolves ilitoka nyuma kwa pointi 16 katika kipindi cha pili na kuwapiga Los Angeles Lakers 112-111 Jumatano usiku katika mchezo wao wa kwanza tangu kifo cha kocha wao  Flip Saunders .

Kevin Martin alifunga pointi 23 kwa Timberwolves siku tatu baada tangu walipompoteza kocha wao Saunders. Kocha wa muda na rais ambaye katika siku za mwisho wake alipigana dhidi ya ugonjwa unaofahamika kama lymphoma Hodgkin .

“Nadhani tulikuwa na msaada kidogo leo,” Rubio alisema. “Imekuwa ni wiki mgumu kwetu, ni vigumu kueleza. Kila mtu akaenda uwanjani  akiwa ni mwenye  maumivu. Lakini, hata kama Flip alitutoka bado atakuwa annaishi na kukaa na sisi milele.”

Timu zote  walivaa nguo za maandalizi ya mchezo ambazo juu yake kulikuwa na maneno ya kumuenzi na  kumuheshimu kocha huyo wazamani wa Timberwolves . Timberwolves yao yalisomeka  kauli mbiu ya ” WE ,” wakati Lakers ‘ yalisema ” FLIP .

Minnesota iliongoza 111-102 kwa 2:11 za mwisho zilizobaki, lakini Lakers walikuja juu na kupata pointi 9-1. Williams alifunga pointi 3 zikisalia sekunde 31 na kuipunguza  Minnesota mpaka  kuongoza kwa pointi moja .

Kobe Bryant alifunga pointi 24 katika mchezo wa kwanza wa msimu wake wa 20 na Lakers.  Amevunja  rekodi ya NBA ya  John Stockton kukaa  kwa misimu mingi na timu moja .

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here