Home Kimataifa JUVENTUS HALI BADO TETE ITALIA

JUVENTUS HALI BADO TETE ITALIA

820
0
SHARE

JuventusHali ya klabu ya Juventus imezidi kuwa mbaya katika Ligi Kuu ya soka nchini Italia baada ya hapo jana kufungwa na klabu ya Sassuolo kwa goli 1-0. Bao la Nicola Sansone mnamo dakika ya 20 lilitosha kuwapa Sassuolo pointi tatu muhimu katika uwanja wake wa nyumbani wa Mapia.

Sassuolo wanashinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Juventus wakiwa wamefungwa michezo minne na kutoka sare mmoja katika michezo yote ya nyumbani na ugenini.

Kwa upande wa Juventus huu unakuwa mwanzo wao mmbaya katika Serie A tangu mwaka 1969.

Nachokiona kwa mtazamo wangu ni kuwa bado mwalimu Massimiliano Allegeri hajaweza kuiunganisha timu katika maeneo yote matatu.Hapa nazungumzia eneo la idara ya ulinzi,kuelekea idara ya kiungo mpaka katika idara ya ushambuliaji.

Ni ukweli usiopingika kuwa kukosekana kwa Pirlo,Vidal na Tevez kumeonekana kuwa pigo kwa klabu ya Juventus lakini lazima maisha yaendelee kama alivyosema Rais wa klabu hiyo Andrea Agnelli katika mkutano wa wanahisa wa klabu ya Juventus kuwa”kuondoka kwa baadhi ya nyota wa klabu hiyo isiwe kisingizio kwa klabu hiyo kufanya vibaya katika michuano mbalimbali.”

Inawezekana maneno ya Agnelli yakalenga upande mmoja wa matumizi makubwa ya fedha kwa kuwasajili baadhi ya wachezaji kuziba nafasi za nyota walioondoka.
Kiasi cha zaidi ya euro milioni 130 kimetumika kuwaleta nyota kama Mario Mandzukic,Paulo Dybala,Mario Lemina,Simone Zaza,Hernanes,Alex Sandro,Juan Cuadrado,Guido Vadala na Sami Khedira.

Kama Juventus wamesajili wachezaji wote hao tatizo lipo wapi?
Tatizo kubwa kwanza kama nilivyosema hapo juu kuwa timu inakosa muunganiko mzuri katika idara zote.Pili si kila mchezaji anayesajiliwa anaweza kuwa na ubora ule ambao unahitajika katika timu.

Mfano msimu uliopita mshambuliaji Alvaro Morata alionekana kuwa nyota wa timu hiyo kwa sababu alikuwa akicheza mbele ya Tevez ambaye kiuhalisia ni mpambanaji na alikuwa kifanya kazi kubwa ya kumpa pasi za mwisho Morata kufunga magoli.

Lakini pia Tevez mwenyewe alikuwa na msaada mkubwa kwa timu yake kutokana na magoli aliyofunga.

Tevez aliweza kuipa Juventus zaidi ya magoli 20 katika michuano yote kitu ambacho kinaonekana kukosekana kwa Juventus hii.Katika idara ya kiungo Pirlo alikuwa ubongo wa timu ya Juventus kwa muda mrefu sana.

Ukiangalia Juventus ya sasa inakosa mtu wa kuiunganisha timu kutoka katika kiungo kuelekea katika ushambuliaji.Pamoja na uwepo wa viungo wa kushambulia kama Hernanez,Pogba,Lemina,Sturaro na Marchisio katika timu hiyo lakini bado nyota hao wameshindwa kuiunganisha timu vizuri kuelekea katika idara ya ushambuliaji.

Idara ya ulinzi nayo ni changamoto kubwa kwa Juventus.Wachezaji Andrea Bazagli,Leonardo Bonnuci na Giorgio Chiellini wanaonekana kuchoka na wanahitaji watu wengine wa kuwasaidia kuifanya Juventus ikaendelea kuwa imara katika idara yao ya ulinzi.

Mpaka sasa Allegri hajui atumie mfumo gani kuweza kuipa Juventus matokeo.Changamoto ya mifumo pia imekuwa kikwazo kwa Juventus kupata matokeo mazuri katika Serie A.Hii imewafanya baadhi ya wachezaji kama Pogba na Paulo Dybala kushindwa kucheza vizuri.

NINI KIFANYIKE.
Inawezekana hiki kikawa kipindi cha mpito kwa Juventus lakini hakuna shaka kuwa bado Juventus wana kikosi kizuri cha kuweza kutoa ushindani katika Serie A.

Kocha Massimiliano Allegri anapaswa kumuamini na kumpa nafasi mshambuliaji Paulo Dybala kuweza kuisadia Juventus kurudi katika ubora wake.Ukiangalia Dybala ndiye mchezaji ghali kwa Juventus kwa msimu huu akinunuliwa kwa kiasi cha euro milini 40 toka Palermo.

Dybala ni mnyumbulifu,ana kasi nzuri ana jicho la tatu la kuona pasi yake ya mwisho iende wapi.Ndio mfungaji bora wa Juventus kwa sasa akiwa na magoli 4 katika Serie A.

Ilinishangaza kumuona akianzia benchi katika michezo mikubwa iliyohitaji watu wa kariba yake dhidi ya Inter Milan katika Serie A na katikati ya juma lililopita katika Ligi ya Maingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach.Hakika Allegri anapaswa kumpa nafasi Dybala.

Pia ni wakati muafaka wa kuanza kumpa nafasi kijana Daniele Rugani kucheza katika idara ya ulinzi.Nyota huyo ametokea klabu ya Empoli na wachambuzi wengi wa soka wanamfananisha na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Fabio Cannavaro.

Rugani anaweza kuwa mbadala mzuri wa beki mkongwe Andrea Bazagli.
Bado Juventus inaweza kutoa ushindani mkubwa katika Ligi ya Italia Serie A.
FORZA SERIE A

Serie A ni moja kati ya Ligi nyingi zinazooyeshwa kupitia Startimes, usijinyime uhondo kukosa kumuona Paul Pogba, Balotelli na mastaa wengine kwenye Serie A.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here