Home Kimataifa GRIFFIN ANG’ARA, CLIPPERS IKIWAPIGA WAFALME WA SACRAMENTO

GRIFFIN ANG’ARA, CLIPPERS IKIWAPIGA WAFALME WA SACRAMENTO

533
0
SHARE

BN

Griffin leo alfajiri alikuwa bora sana akiiongoza Clippers kupata ushindi dhidi ya Sacramento  Kings 111-104 . Pamoja na mchezo kuwa  katika usawa katika dakika za mwisho , Paul  Pierce alifanya kile ambacho  Clippers Los Angeles walitarajia  angeweza kufanya katika  zile sekunde za mwisho za mchezo.

Alifunga pointi za mwisho zilizowaweka mbele na hii  ikizoeleka hivi kipindi  akiwa na vilabu vya Bosto Cletics na Washington Wizards. Hiyo ndio sababu  ya yeye kuwepo hapa, ” nahodha na point guard Chris Paul alisema.

Kundi hili limekuwa pamoja kwa miaka kadhaa , wana uelewano  mzuri wa kila mmoja na mwingine, ” Pierce alisema. ” Mimi n inachojaribu kufanya nikufit katika kundi hili  na kucheza nao katika namna iliyonyooka na sawia. Blake Griffin aliongoza njia na pointi 33 na Paul aliongeza pointi 18 na pasi 11 .

Clippers ilipoteza uongozi wa pointi 15 kabla ya kunusurika mwishoni na kwenda  kushinda . DeMarcus Cousins  alikuwa na pointi 32 na rebound 13 kwa Sacramento  Kings. Huu ukiwa ndio msimu wao wa mwisho katika uwanja wa Sleep Train Arena.

Rudy Gay  alirudi katika  timu muda mfupi kabla ya mchezo baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa pili Jumatatu. Alianza na alifunga pointi 16 . … Kings wamepoteza michezo sita ya  nyumbani dhidi Clippers .

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here