Home Kitaifa AZAM YAKWEA KILELENI RASMI, KAVUMBAGU ADHIHIRISHA UBORA WAKE

AZAM YAKWEA KILELENI RASMI, KAVUMBAGU ADHIHIRISHA UBORA WAKE

585
0
SHARE
Didier Kavumbagu akishangilia goli lake baada ya kufunga dhidi ya JKT Ruvu
Didier Kavumbagu akishangilia goli lake baada ya kufunga dhidi ya JKT Ruvu
Didier Kavumbagu akishangilia goli lake baada ya kufunga dhidi ya JKT Ruvu

Mabingwa wa kombe la Kagame Azam FC wamefanikiwa kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Azam wamefikisha jumla ya pointi 22 na kuiacha Yanga ikisalia nafasi ya pili ikiwa na pointi 20 baada ya jana kulazimishwa sare ya kufungana kwa goli 2-2 dhidi ya Mwadui FC.

Azam vs Ruvu 3

Didier Kavumbagu alianza kuifungia Azam goli la kwanza dakika ya nne ya mchezo baada ya kumtoka beki wa JKT Ruvu Renatus Morris na kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa JKT Ruvu Shabani Dihile.

Goli la pili la Azam limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya sita baada ya uzembe wa mabeki wa JKT Ruvu kujichanganya katika kumdhibiti Bocco ambaye aliachia kiki iliyomshinda Dihile na kujaa moja kwa moja kambani.

Azam vs Ruvu 4

Kabla ya kwenda mapumziko, Najim Magulu aliifungia JKT Ruvu goli la kwanza baada ya kutokea piga-nikupige kwenye lango la Azam FC. Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Azam wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza, JKT Ruvu walifanya shambulio kali kwenye goli la Azam lakini beki wa Azam Agrey Morris aliokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni.

Azam vs Ruvu

John Bocco alipachika goli la tatu kwa upande wa Azam kwa mkwaju wa penati kufuatia Shomari Kapombe kuangushwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuamuru ipigwe penati.

Samwel Kamuntu akaifungia JKT Ruvu goli la pili dakika ya 64 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Azam kupata ushindi wa goli 4-2 dhidi ya JKT Ruvu.

Azam vs Ruvu 5

Wakati kila mtu akisubiri mwamuzi apulize filimbi ya mwisho kwa kuamini mchezo huo unamalizika kwa Azam kushinda kwa goli 3-2 dhidi ya Ruvu, Kipre Tchetche aliyeingia kuchukua nafasi ya Bocco alifunga goli la nne kwa upande wa Azam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here