Home Kimataifa CAVALIERS YAIPA KUBWA MEMPHIS GRIZZLIES

CAVALIERS YAIPA KUBWA MEMPHIS GRIZZLIES

522
0
SHARE

cavsKevin Love alikuwa na pointi 17 na 13 rebounds , Richard Jefferson alikuwa na pointi 14 na Cleveland kupata faida kubwa mapema na kuibamiza  Grizzlies iliyokuwa ovyo kabisa  kwa jumla ya pointi  106-76.

Cleveland walinufaika na kiwango kibovu cha urushaji mipira cha Memphis khali iliyopelekea kupata uongozi mapema tu katika robo ya kwanza. Waliongeza uongozi wao mpaka kufikia tofauti ya pointi kuwa 32 katika robo ya nne ya mchezo. Cavaliers walipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Chicago  Bulls 97-95 Jumanne usiku .

LeBron James , Jared Cunningham na Mathew Dellavedova walikuwa na pointi 12 kila moja , huku Lebron akishuhudia moja ya siku zake mbaya za ufungaji kwani alipata mitupo 4 tu kati ya 12 aliyojaribu.

Zach Randolph na Marc Gasol wao waliiongoza Memphis  Grizzlies kwa kufunga  pointi 12 kila moja .

“Hiyo ndio  namna tunahitaji kuwa ,” James alisema juu ya ulinzi. “Hao ndo sisi sasa.. Ili tuwe wale ambao tunataka kuwa , inabidi kuendelea kuwa na ulinzi imara na ulio katika ngazi ya juu.

HIGHLIGHTS

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here