Home Ligi EPL ZINEDINE ZIDANE AMEKATAA KUMFANANISHA MARTIAL NA THIERRY HENRY

ZINEDINE ZIDANE AMEKATAA KUMFANANISHA MARTIAL NA THIERRY HENRY

610
0
SHARE

sdfgghf

Mchezaji wa zamani wa Monaco Anthony Martial ambae hivi sasa anachezea Manchester united amekua akifananishwa sana na Thierry Henry mchezoni.

Lakini mkongwe Zidane amekataa kumfananisha Martial na Henry. Kwanza kabisa Zidane aliongelea kuhusu gharama ya uhamisho wake,“Kuhusu swala la gharama ya uhamisho wake unaweza kudhani kama mwaka umepita sasa hivi kwasababu hakuna anaezungumzia hilo swala tena”

“Nakumbuka watu waliongea sana kuhusu Gainluigi Buffon kununuliwa kwa pesa nyingi na Juventus na kusema kwamba tangu lini kipa akanunuliwa kwa gharama hiyo. Lakini mwisho wa siku nani anaendelea kuzungumzia gharama ya Buffon sasa hivi”

“Mfano mwingine ni pesa zilizolipwa kwa ajili ya Ronaldo, baada ya magoli yaliyofungwa hakuna tena mtu anayeweza kuzungumzia pesa”

Kuhusu Martial kufananishwa na Henry alisema, “Hapana, Henry ni mmoja kati ya wachezaji bora na sio sawa kumfananisha na Martial kwa sasa. Pia sio vizuri kumpa pressure Martial kwamba yeye anafanana na Henry wakati bado ni mdogo na ana uwezo na ajiamini vizuri uwanjani. Tuendelee kumuacha acheze kwasababu ana future nzuri mbele yake”

during the UEFA Champions League Group B match between Manchester United FC and VfL Wolfsburg at Old Trafford on September 30, 2015 in Manchester, United Kingdom.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here