Home Kitaifa MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA VPL ZILIZOCHEZWA JUMATANO

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA VPL ZILIZOCHEZWA JUMATANO

691
0
SHARE

VPL-Tanzania

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea kwenye viwanja kadhaa na kushuhudia timu zikipata matokeo tofauti wakati zilipokuwa zikiwania pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Mwadui FC imeipunguza kasi Yanga sc baada ya kuilazimisha sare ya kufungana bao 2-2.

Mabao yote mawili ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zimbabwe Donald Ngoma wakati mabao ya Mwadui yakifungwa na Paul Nonga na Bakar Kigodeko.

Mtibwa Sugar wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani (Manungu) Turiani, mkoani Morogoro kwa kuwafunga nduguzao Kagera Sugar kwa goli 1-0.

Majimaji wakiwa ugenini wamefanikiwa kulazimisha sare ya kufungana kwa goli 1-1 dhidi ya wenyeji wao Mbeya City kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya.

Katika mchezo huo, Majimaji ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Samir Luhava lakini Mbeya City wakasawazisha kwa mkwaju wa penati mfungaji akiwa ni Raphael Alfa.

Kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, Ndanda FC wamelazimishwa suluhu na Stand United ‘Chama la wana’ kutoka Shinyanga.

Timu ya Toto Africans ‘wana-kishamapanda’ wamefanikiwa kupata pointi tatu katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Mgambo Shooting kwa goli 1-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Goli pekee la Toto Africans limefungwa na Miraji Athumani kwa mkwaju wa penati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here