Home Kimataifa LEBRON AREJEA, CLEVELAND CAVS IKIPIGWA NA CHICAGO BULLS

LEBRON AREJEA, CLEVELAND CAVS IKIPIGWA NA CHICAGO BULLS

455
0
SHARE

Sio kila ukiwa na tatizo katika ufungaji basi huwezi kutoa msaada katika timu yako ili upate ushindi. hayoo ndiyo maneno unayoweza kusema juu ya mchezaji wa Chicago Bulls, Paul Gasol ambaye alitarajiwa pengine angekuwa na siku nzuri hasa baada ya kutoka kuwa MVP wa mashindano ya Ulaya kwa mataifa ambako aliiongoza Hispania kushinda taji. lakini khali ilikuwa tofauti kwa mchezo wa jana kwani alishindwa kabisa kuwa na shabaha ya kufunga vikapu kama ilivyozoeleka lakini msaada wake katika ulinzi ulichangia ambapo block yake moja ya mwisho zikiwa zimesalia sekunde takribani 4 kwa Lebron ndio iliiokoa mchezo huo. Hiyo ilikuwa block yake ya 6 ya mchezo huo.

Akicheza kwa muda maalumu uliodhibitiwa kutokana na ushauri wa madaktari hasa baada ya kuchomwa sindano kutokana na matatizo ya mgongo Lebron James aliiongoza Cleveland kwa kufunga vikapu 25 na kudaka rebound 10, huku mchezaji aliyerejea kutokana na kukosekana kwa hatua ya myoano ya msimu uliopita Kevin Love vikapu 18 na huyu ndiye aliyewarejesha cleveland mchezoni baada ya kufunga point 3 mara mbili mfululizo katika dakika ya mwisho. Mo Williams aliyeanza nafasi ya Kyrie Irving aliyekuwa majeruhi kutokana na kuumia goti alifunga point 19 na kutoa assist 7.

Kwa Upande wa Chicago Bulls, kocha kijana huyu ambaye yupo katika mwaka wake wa kwanza Hoiberg aliwashangaza wengi baada ya kumuacha katika benchi Joakhim Noah na kumuanzisha Mirotic katika nafasi yake. lakini kubwa kuna mabadiliko yameonekana nayo ni aina ya ushambuliaji ambayo sasa Chicago wanashambulia kwa uwazi zaidi kuliko alivyokuwepo Thom Thibodeau.

Derrick Rose alifunga pointi 18, Nikola Mirotic akafunga pointi 19 na Jimmy Butler alifunga pointi 17 na kupokonya mipira miwili.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here