Home Ligi KIIZA AREJEA KUTOKA MAJERUHI NA KUTUPIA NYAVUNI, SIMBA IKIPATA POINTI 3

KIIZA AREJEA KUTOKA MAJERUHI NA KUTUPIA NYAVUNI, SIMBA IKIPATA POINTI 3

783
0
SHARE
Hamisi Kiiza (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Simba baada kufunga goli dhidi ya Coastal Union
Hamisi Kiiza (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada kufunga goli dhidi ya Coastal Union
Hamisi Kiiza (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada kufunga goli dhidi ya Coastal Union

Hamisi Kiiza ameifungia Simba goli pekee kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Coastal Union mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Hamisi Kiiza akidhibitiwa vyema na mlinzi wa Coastal Union
Hamisi Kiiza akidhibitiwa vyema na mlinzi wa Coastal Union

Kiiza aliyerejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi na kukosa mechi tatu, alifunga goli hilo dakika ya tisa kipindi cha kwanza akiunganisha krosi iliyopigwa na mlinzi wa kulia wa Simba Ramadhani Kessy.

Mshambuliaji wa Simba SC Hamisi Kiiza akishangila goli aliloifungia timu yake dhidi ya Coastal Union
Mshambuliaji wa Simba SC Hamisi Kiiza akishangila goli aliloifungia timu yake dhidi ya Coastal Union

Simba bado wameendelea kukabiliwa na tatizo la kukosa magoli ambapo kwenye mchezo wa leo kama wangekuwa makini wangeibuka na ushindi mnono kuliko walioupata dhidi ya Coastal Union.

Simba vs Coastal 2Kipindi cha pili Coastal Union walibadili aina uchezaji kwa kuanza kucheza mipira mirefu na kushambulia kwa kushtukiza. Kikosi hicho ambacho kinanolewa na kocha Jackson Mayanja kitajilaumu kwa kupoteza nafasi za wazi zikiwa ni dakika za majeruhi.

Simba vs Coastal 3

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here