Home Kimataifa GOLDEN STATE WARRIORS YAANZA VYEMA, CURRY HAKAMATIKI

GOLDEN STATE WARRIORS YAANZA VYEMA, CURRY HAKAMATIKI

585
0
SHARE

Katika uwanja wa Oakland Arena nyumbani kwa Golden State warriors, mambo kadhaa yalijitokeza lakini kubwa kuliko yote ilikuwa ni matukio mawili ambayo ni kusimikwa kwa bango jipya ndani ya uwanja huo ambayo ni utamaduni wa NBA, timu inayoshinda ubingwa kupandisha bango ukutani ambalo huonyesha mafanikio ya msimu uliomalizika.

Stephen Curry ambaye ndiye nahodha wa imu hiyo aliongoza kwa neno na kutoa shukrani kwa mashabiki na wachezaji waliohama ambao pia walichangia kwa kiasi kikubwa ushindi huo wa kihistoria baada ya miaka 40, kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1975.

Lakini kabla ya kupandishwa kwa Bango hilo kamishna wa NBA, David Sliver aliongoza ugawaji wa Pete maalumu za ushindi wa taji hilo kubwa zaidi katika mchezo wa kikapu duniani, ambapo  tofauti na michezo mingine, NBA hutoa pete badala ya Medali.

Katika kuonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali, Stephen Curyy aliiongoza Golden State warriors kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya timu inayofundishwa na aliyekuwa kocha wao msaidizi msimu uliopita Alvin Gentry ambaye naye alipokea pete yake jana, timu ya New Orleans Pelicans. curry alianza kwa kasi mchezo huo akifunga point 24 katika robo ya kwanza ya mchezo kabla ya kumaliza na pointi 40 na Golden kushinda kwa pointi 95-111.

mchezaji anayetazamiwa kwa na msimu bora Anthony Davis alikuwa na moja ya siku mbaya baada ya kufunga pointi 18 pekee huku akipata mitupo 4 tu kati ya 20.

hii inakuwa mara ya kwanza baada ya maiaka kwa mchezaji kufunga zaidi ya pointi 20 katika robo ya kwanza ya mchezo siku ya ufunguzi au mechi ya kwanza.

MATOKEO KATIKA PICHA

CC

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here