Home Kimataifa CHELSEA HOI TENA…YAVULIWA UBINGWA NA STOKE CITY

CHELSEA HOI TENA…YAVULIWA UBINGWA NA STOKE CITY

932
0
SHARE

Chelsea hoi 1

Jose Mourinho ameendelea kuwa katika wakati mgumu katika kipindi hiki baada ya kikosi chake cha Chelsea kupoteza mchezo wa kombe la Capital One mbele ya Stoke City na kuondoshwa kwenye michuano hiyo usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano.

Stoke City wamesogea kwenye raundi ya tano ya michiuano hiyo kwa ushindi wa penati 5-4 kufuatia sare ya kufungana goli 1-1.

chelsea hoi 3

Jonathan Walters alianza kuifungia goli la kuongoza Stoke City dakika chache baada kipindi cha pili lakini Loic Remy aliyeingia kuchua nafasi ya Diego Costa aliyetoka baada ya kuumia, akaiswazia goli Chelsea dakika ya 90 ya mchezo.

Chelsea ilishindwa kutumia vyema pengo lililoachwa na Phil Bardsley aliyeoneshwa kadi nyekundu dakika ya tisini na kuifanya Stoke City kucheza pungufu dakika zote 30 za nyongeza kumtafuta bingwa wa mchezo huo.

Chelsea hoi 2

Winga wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard alikosa penati iliyoifanya Chelsea kutupwa nje ya mashindano hayo.

Kuvuliwa huku kwa ubingwa huu wa Chelsea ni habari mbaya kwa kocha Jose Mourinho ambaye hana raha na sasa ana subiri hatima yake dhidi ya Liverpool Jumamosi ijayo kuona kama ataendelea kuwa meneja wa Chelsea.

Stoke City (4-2-3-1): Butland, Bardsley, Shawcross, Wollscheid, Muniesa (Wilson 49), Whelan, Adam, Diouf, Afellay (Shaqiri 76), Arnautovic, Walters (Odemwingie 90)

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Ireland, Sidwell, Given, Crouch

Kadi za njano: Bardsley, Wilson

Kadi nyekundu: Bardsley

Mfungaji wa goli: Walters 52

Kocha: Mark Hughes 7

chelsea hoi 5

Chelsea (4-2-3-1): Begovic, Zouma, Cahill, Terry, Baba (Kenedy 67), Ramires (Traore 80), Mikel, Willian, Oscar, Hazard, Costa (Remy 33)

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Djilobodji, Azpilicueta, Amelia, Loftus-Cheek

Kadi ya njano: Baba

Mfungaji wa goli: Remy 90

Kocha: Jose Mourinho 7

chelsea hoi 4

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here